KINARA WA ‘ASISST’ VPL 2014/15 ASISITIZA HATOJIUNGA NA TIMU YAKE HADI KIELEWEKE


VPL-Tanzania
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Kiungo mshambuliaji wa kati, Abdallah Seseme bado hajajiunga na klabu yake ya Toto Africans ya Mwanza licha ya timu hiyo kuanza mazoezi wiki hii. Seseme mchezaji wa zamani wa Simba SC amecheza mechi zote 10 za klabu yake msimu huu katika ligi kuu na kuisaidia kukusanya alama 13 huku wakiwa nafasi ya 8 kati ya timu 16.
Toto watakuwa wageni wa Majimaji FC katika uwanja wa Majimaji, Songea tarehe 12 mwezi ujao lakini Seseme anasema kuwa atajiunga hivi karibuni na timu yake baada ya uongozi kukamalizana naye. Mchezaji huyo bado anadai sehemu ya fedha zake za usajili na anaona ni bora amalizane kabisa na timu hiyo katika madai waliyokubaliana wakati wa usajili.
“Bado sijajiunga na timu. Kuna baadhi ya mambo nasubiri uongozi unikamilishie, si unajua tena tunaingia lala salama kwa hiyo ni lazima kujua mapema mwelekeo wangu”, anaanza kusema mchezaji huyo aliyecheza mechi zote za timu yake na ku-asisst magoli manne kati ya 6 yaliyofungwa na timu yake hadi ligi inasimama.
Toto Africans inataraji kufanya harambee kubwa ya kusaka zaidi ya shilingi milioni 200 ili kusaidia uendeshaji wa timu hiyo, kulipa mishahara, posho na kusaidia mahitaji muhimu ya timu. Tangu kuanza kwa msimu timu hiyo ya Mwanza imekuwa ikilia ukata. Jambo hilo ni tatizo kwa timu yoyote ile lakini Seseme anasema kwamba wachezaji vijana hawakujali sana hali hiyo.
“Ni kweli hali haikuwa nzuri sana lakini wachezaji wengi vijana halikuwa tatizo kubwa kwetu. Nafikiria upande wa uongozi ndiyo kulikuwa na tatizo ndiyo sababu ya timu kuwa na kiwango cha kupanda na kushuka.
“Wachezaji tumejiwekea malengo lakini tulikuwa tukikwamishwa na uongozi kwa maana haukuoneka kuwa na malengo yanayoendana na wachezaji”, alisema Seseme wakati alipofanya mahojiano mafupi na mtandao huu Alhamis hii.



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: