EL CLASICO-KIPIGO REAL: BENITEZ ANUSURIKA SHOKA, PEREZ AKANA MAASI YA RONALDO NA WENZAKE!



REAL-BENITEZ2RAIS wa Real Madrid Florentino Perez amesisitiza katika Mkutano na Wanahabari
aliouitisha Jana huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid kuwa Kocha Rafa Benitez atabaki kazini licha ya Jumamosi kutandikwa 4-0 na Barcelona kwenye El Clasico iliyochezwa Nyumbani kwao hapo hapo Bernabeu.
Wakati Real inacharangwa na Barca Juzi Jumamosi, Mashabiki wa Real waliokuwepo Uwanjani Bernabeu walimtaka Perez huku Wadau wengi wakimlaumu kwa kuingilia upangaji Timu na kung’ang’ania kuchezeshwa Wachezaji wakubwa hata kama wamedorora na kuachwa Wachezaji ambao wako kwenye fomu.
Mwaka 2006, Mashabiki walimgeukia na kumsakama Perez ambae ghafla alibwaga manyanga na kuachia wadhifa wake wa Urais.
Mkutano huo na Wanahabari umekuja baada ya mapema Jana Bodi ya Real kuketi kutafakari kipigo chao kutoka kwa Barca.
Ushindi wa Barca wa Jumamosi umewafanya wawe Pointi 6 kileleni mbele ya Real ambao wameporomoka hadi Nafasi ya 3 baada ya Atletico Madrid Jumapili kuifunga Real Betis 1-0 na kushika Nafasi ya Pili.
Benitez, aliewahi kuzifundisha Valencia, Liverpool, Inter Milan, Chelsea na Napoli, ni Meneja wa 10 chini ya himaya ya Perez na alitwaa wadhifa huo mwishoni mwa Msimu uliopita kutoka kwa Carlo Ancelotti.
Katika Mkutano huo Perez alisema Bodi ya Real bado ina imani na Benitez licha ya kupata matokeo mabaya na Barcelona.
Vile vile, Perez alikanusha kuwepo mgomo wa Wachezaji ambao hawamtaki Benitez wakiongozwa na Cristiano Ronaldo na kusisitiza hamna kitu kama hicho.
Mechi inayofuata kwa Real ni hapo Jumatano Ugenini huko Ukraine wakicheza na Shakhtar Donetsk katika Mechi ya Kundi A la UEFA CHAMPIONZ LIGI ambao wao washafuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 huku wakiwa na Mechi 2 mkononi.
Ikiwa Real wataifunga Shakhtar basi watajihakikishia kufuzu toka Kundi A wakiwa ndio Vinara.


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: