CECAFA CHALENJI CUP 2015: KILI YAITWANGA RWANDA, ZENJI YATWANGWA NA UGANDA!



CECAFA2015MECHI za CECAFA CHALENJI CUP zimeendelea Leo huko Ethiopia ambapo Zanzibar ilifungwa 4-0 na Uganda na kisha Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, kucheza huko Mjini Awassa na Rwanda na kushinda 2-1 na kupaa kileleni mwa Kundi A.
Kilimanjaro Stars walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 23 kupitia Said Ndemla na Bao hilo kudumu hadi Mapumziko.
Katika Dakika ya 77, Simon Msuva aliipa Kili Stars Bao la Pili na kuongoza 2-0 lakini Rwanda walifunga Bao lao pekee Dakika ya 89 kupitia kupitia Tisiyege..
Hadi Mechi inakwisha Kili Stars 2 Rwanda 1 na ushindi huu umewaweka Kili kileleni mwa Kundi A wakiwa na Pointi 6 kwa Mechi 2.
Katika Mechi ya awali, Uganda waliitwanga Zanzibar 4-0 katika Mechi ya Kundi B.
Bao za Uganda, ambao walichapwa 2-0 na Kenya katika Mechi yao ya kwanza, zilifungwa na Farouk Miya na Erisa Ssekisambu, kila mmoja akipiga Bao 2, huku moja la Erisa Ssekisambu likiwa la Penati baada ya Kipa Ali Mwadini kucheza Faulo na kupewa Kadi Nyekundu.
Zanzibar walibaki Mtu 9 kwa Robo ya Saa ya mwisho baada ya Yahaya Mudathir kupewa Kadi Nyekundu.
Zanzibar wamebakisha Mechi 1 ya Kundi B ambayo watamaliza na Kenya hapo Ijumaa huku pia Kili Stars wakibakisha 1 dhidi ya Wenyeji Ethiopia hapo Jumamosi.
KIKOSI CHA KILI STARS:
Aishi Manula,Shomari Kapombe,Mohamed Hussein,Salim Mbonde,Kelvin Yondani,Himid Mao,Saimon Msuva,Said Ndemla,John Bocco,Elias Maguri,Deus Kaseke.
Akiba:Ally Mustafa, Kessy Ramadhani, Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Salum Telela,Salum Abubakar, Malimi Busungu
CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP 2015
MSIMAMO

KUNDI A
NR
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Kili Stars
2
2
0
0
6
1
5
6
2
Rwanda
2
1
0
1
2
2
0
3
3
Ethiopia
1
0
0
1
0
1
-1
0
4
Somalia
1
0
0
1
0
4
-4
0

KUNDI B
NR
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Uganda
2
1
0
1
4
2
2
3
2
Kenya
1
1
0
0
2
0
2
3
3
Burundi
1
1
0
0
1
0
1
3
4
Zanzibar
2
0
0
2
0
5
-5
0

KUNDI C
NR
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
South Sudan
1
1
0
0
2
0
2
3
2
Malawi
1
1
0
0
2
1
1
3
3
Sudan
1
0
0
1
1
2
-1
0
4
Djibouti
1
0
0
1
0
2
-2
0
**Timu 2 za juu toka kila Kundi na Washindi Watatu wawili bora watasonga Robo Fainali
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
**Saa: Mechi ya Kwanza Saa 10 na ya Pili Saa 12
Jumamosi Novemba 21
Burundi 1 Zanzibar 0
Ethiopia 0 Rwanda 1
Jumapili Novemba 22
Somalia 0 Tanzania 4
Kenya 2 Uganda 0
Jumatatu Novemba 23
South Sudan 2 Djbouti 0
Sudan 1 Malawi 2
Jumanne Novemba 24
Zanzibar 0 Uganda 4
Rwanda 1 Tanzania 2
Jumatano Novemba 25
Kenya Vs Burundi
Somalia Vs Ethiopia
Malawi v Djibouti
South Sudan v Sudan
Ijumaa Novemba 27Rwanda Vs Somalia
Zanzibar Vs Kenya
South Sudan v Malawi
Djibouti V Sudan
Jumamosi Novemba 28Uganda Vs Burundi
Tanzania Vs Ethiopia
Robo Fainali
Jumatatu Novemba 30
B1 Vs C2 [19]
A1 Vs best Q2 [20]
Jumanne Desemba 1
C1 Vs best Q2 [21]
A2 Vs B2 [22]
Nusu Fainali
Alhamisi Desemba 3
Mshindi 19 Vs Mshindi 20

Mshindi 21 Vs Mshindi 22
Jumamosi Desemba 5
Mshindi wa Tatu
Fainali



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: