Mwaka Jana, Straika wa Yanga, Mrisho Ngassa, alikuwa mmoja wa Wachezaji Wanne waliofungana kwa Bao 6 kila mmoja katika Listi ya Wafungaji Bora wa CAF CHAMPIONZ LIGI.
Mwaka huu Mtanzania mwingine, Mbwana Samatta, ndie anaongoza katika Ufungaji Bora wa CAF CHAMPIONZ LIGI akiwa na Bao 7 baada ya Jumamosi kufunga Bao la Pili na la ushindi huko Algiers, Algeria wakati Klabu yake TP Mazembe inaichapa USM Alger Bao 2-1 katika Mechi ya Kwanza ya Fainali za CAF CHAMPIONZ LIGI kwa Mwaka huu.
Timu hizi zitarudiana Jumapili ijayo huko Lubumbashi Nchini Congo DR na Mshindi kuibuka ndio Klabu Bingwa ya Afrika na kuzoa kitita cha Dola Milioni 1.5 pamoja na kuiwakilisha Afrika katika Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani Mwezi Desemba huko Japan.
Kwenye mbio hizi za Buti ya Dhahabu, Samatta anakimbizwa na Mchezaji mwenzake wa TP Mazembe Roger Assale mwenye Bao 5 na pia wapo Wachezaji Watatu wa USM Alger ambao wana Bao 3 kila mmoja ambao wanaweza kumpiku Samatta.
Wachezaji hao ni Youcef Belaili, Kadour Beljilali na Mohamed Meftah.
CAF CHAMPIONZ LIGI
FAINALI
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 31
Union Sportive Medina d’Alger [Algeria] 1 TP Mazembe [Congo, DR] 2
Marudiano
Jumapili Novemba 8
1630 TP Mazembe v Union Sportive Medina d’Alger
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment