Timu hizo za Ligi Kuu England, kuanzia Liverpool ambayo Msimu uliopita walitoka Sare na safari ikaifunga Chelsea 3-1 hapo Juzi, nyingine ni Stoke City, Norwich City na Tottenham.
Mechi nyingine za Chelsea kwa Mwezi huu Novemba ni mbili za Kundi G la UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Dynamo Kiev, ambayo walitoka nayo 0-0 kwenye Mechi ya Kwanza, na nyingine na Maccabi Tel Aviv ambayo waliichapa 4-0.
+++++++++++++++++++++++++++++++
Chelsea – Mechi zijazo:
UEFA CHAMPIONZ LIGI-Kundi G
Jumatano Novemba 4
2245 Chelsea v Dynamo Kiev
LIGI KUU ENGLAND
Jumamosi Novemba 7
2030 Stoke v Chelsea
LIGI KUU ENGLAND
Jumamosi Novemba 21
1800 Chelsea v Norwich
UEFA CHAMPIONZ LIGI-Kundi G
Jumanne Novemba 24
2245 Maccabi Tel-Aviv v Chelsea
LIGI KUU ENGLAND
Jumapili Novemba 29
1500 Tottenham v Chelsea
+++++++++++++++++++++++++++++++
Akisakamwa na matokeo mabovu yaliyomtupa Nafasi ya 15 kwenye Ligi wakiwa Pointi 14 nyuma ya Vinara Man City baada ya Mechi 11 ambazo Wameshinda 3, Sare 2 na Kufungwa 6, Jose Mourinho yuko taabani hasa kwa vile Chelsea ndio Mabingwa Watetezi.
Mwezi huu Novemba kwenye Ligi, watacheza Ugenini na Stoke City ambayo Msimu uliopita walitoka Sare 1-1 kisha kucheza Nyumbani na Norwich City ambayo nayo walitoka nayo Sare 0-0 na kumalizia na Tottenham ambayo Msimu uliopita iliibamiza Chelsea 5-3.
@ SOKA IN TANZANIA
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment