Aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu ya Simba SC Selemani Matola, siku chache zijazo huenda akajiunga na timu ya Geita Gold FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara.
November 11 mwaka huu, Matola aliandika barua kwa ajili ya kuomba kujiuzulu kukifundisha kikosi cha Simba kwa madai kuwa hana maelewano mazuri na kocha mkuu Dylan Kerr.
Matola amekuwa kocha msaidizi kwenye kikosi cha Simba kwa muda mrefu baada ya kuitumikia Simba kama mchezaji na nahodha pia.
Geita Gold FC ipo kundi C na inashika nafasi ya pili kwenye kundi hilo ikiwa na pointi 12 nyuma ya JKT Oljoro inayoongoza kundi hilo ikiwa na kileleni kwa pointi 14.
Kwenye kundi C kuna timu za Geita Gold FC, JKT Oljoro, Polisi Tabora, Panone FC, Mbao FC, Rhino Rangers, Polisi Mara na JKT Kanembwa.
Baada ya kutua kwenye kikosi hicho Matola atakuwa na kazi ya kuhakikisha anakisaidia kupanda daraja kwa ajili ya kushiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment