TAHADHARI YA OBAMA KWA KANYE WEST JUU YA KUWANIA URAIS WA MAREKANI

 
Rais wa Marekani Barack Obama emetumia ukumbi wa kukusanya fedha kukejeli nia ya rappa Kanye West kuwania urais 2020.
Obama ambaye yuko San Francisco amemtahadharisha mwanamuziki huyo wa mtindo wa kufoka (Rap) kuwa sharti awatarajie watu wanaoishi maisha yao ni kama wale wasanii wanaoishi maisha yao yote kwenye show ya TV.
Kanye West, alitangaza majuzi tu kuwa atawania urais wa Marekani mwaka wa 2020.
Rais Obama alinukuu ule wimbo wa 'Beautiful Dark Twisted Fantasy' na kumuonya atahadhari dhidi ya kuropokwa tu asije akawaudhi wapiga kura.
Obama alimuonya kuwa heri ateleze aanguke lakini asiteleze ulimi kama wabunge kadhaa wa bunge la Congress la Marekani ambao wamepoteza nyadhfa zao baada ya kuteleza ulimi.
''sharti uwe tayari kukabiliana na watu wenye kuishi maisha yao kama wasanii kwenye shoo za moja kwa moja''alisema Obama.
Hata hivyo wachanganuzi wa maswala ya siasa wanashuku kuwa ujumbe huo wa Obama haukumlenga rappa Kanye West ila muaniaji kiti cha urais wa chama cha Republican Donald Trump.


Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: