MUZIKI .TULIPO TOKA MZIKI WA DANCE ZILIPENDWA

 Tokeo la picha la historia mziki wa zamani tanzania

 Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.......


Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba,Hekaheka,Heka koka,Watoto wa nyumbani,Air Pambamoto(awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.....

Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa......Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku,Mary Maria,Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuw a lifti,Tambiko la Pambamoto,Adza(Aza),Ngapulila, Ogopa Tapeli,Mwisho wa Mwezi,Penzi haligawanyiki,Wivu,Malaine,Nyo ngise,Shoga,Theresa,V.I.P,Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu....

Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku',Hamza Kalala 'Komando',Manitu Mussa,Issa Chikupele,Hassan Dalali,Hassan Shaw,Ally Jamwaka,Abuu Semhando,Bakari 'Baker' Semhando,Mhina Panduka 'Toto Tundu',Adam Bakari 'Sauti ya zege',Eddy Sheggy,Shaban Yohana 'Wanted',Rashid Pembe 'Profesa',Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo,John Kitime,Abdallah Mgonahazelu,Freddy Benjamin,Mohammed Gotagota,Said Hamis 'Misukosuko',Athumani Momba na wengine kibao


 Bila kuwasahau wataalam wa Tatunane.....

Hawa jamaa walikuwa wakiupiga muziki wetu wa asili kwa kutumia ala/vyombo vya kisasa.....Hawa waliutangaza sana muziki wetu nje ya nchi(hasa Denmark na Uholanzi) ambako walikuwa wakifanya maonesho ya mara kwa mara....

Bendi hii iliundwa na wa wanamuziki kama Omary Naliene(mtaalamu wa kucheza ngoma,kupiga marimba,kuimba na kupuliza filimbi huyu,alikuwa anapuliza filimbi kwa pua), Charles Mhuto(Mpiga drums), Mahdi Tumbo(Mpiga gitaa la solo na muimbaji), Seif Rengwe(Mpuliza trumpet), Teddy Mbaraka(Mpiga gitaa la besi na muimbaji), Omary Abdallah Dulla Mnanga(Mpiga ngoma na muimbaji) na Kipara Yusuph(Mpiga ngoma)

Bendi hii ilitamba na nyimbo kama Kulalama,Sangula,Msewe,Wasknai a,Furahia ngoma,Utamaduni,Pili, Naukala,Dunia, Tanzania, Dogoli, Zanzibar, Mangaka, Juma ndala, Kala hasara, Mdundiko, Filimbi, Ludewa na nyingine nyingi ambazo ziliitangaza nchi yetu katika medani ya muziki wa kimataifa...


 Wimbo huu uliimbwa na Orch. Marquis Original na baadae kurudiwa na Nguza Vicking(Babu Seya) akiwa kama mwanamuziki wa kujitegema(solo artist)....Mashairi ya wimbo huu yako hivi: ....

Kama wewe umenipenda kwa nini kunidanganya bwana wee,
Kujibandika madaraka sio yako bwana wewe,
Kama wewe umenipenda kwa nini kunidanganya bwana wee,
Kujibandika madaraka sio yako bwana wewe,

Nimesikia tetesi kuwa huna lolote hata kazi huna ee,
Unazurura mchana kutwa ee,kupita kurandaranda mitaani,
Nimesikia tetesi kuwa huna lolote hata kazi huna ee,
Unazurura mchana kutwa ee,kupita kurandaranda mitaani,

Kumbe hukuwa na uwezo wa kunioa ila kuniharibia maisha,
Heri unaimbie ukweli ulivyo kuliko kunidanganya,

Nikuelewe vipi ee babu ee unaminifu wako uko wapi ee,babaa,
Nikuelewe vipi ee babu ee unaminifu wako uko wapi ee,babaa

Bridge: (Nguza) Karubandika..........Kumbe wewe tapeli

Nikuelewe vipi ee babu ee unaminifu wako uko wapi ee,babaa,
Nikuelewe vipi ee babu ee unaminifu wako uko wapi ee,babaaaaaaaaaaaa

Usinione bweg baba,usinione bweg baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....
Usinione bweg baba,usinione bweg baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....


(Nguza); Nilitaka kujitumbukiza ndani ya moto mie,kumbe bwana yule hana kitanda wala shuka,pa kulala hana analala kwenye stendi ya basi,pa kulala hana anakesha kwenye kituo cha City,Karubandika yoyo,acha vituko we baba....


Usinione bweg baba(Karubandika yoo),usinione bweg baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....

(Nguza); Akiingia kwenye baa kazi yake kuomba bia,akiingia kwenye bia kazi yake kuomba baa,hana hata aibu ee,sigara pia anaomba,hana hata aibu wee na supu pia anabomu,mitaani na kwenye masoko kujitangazia kuwa yeye ni mkurugenzi wa kampuni fulani,kumbe sio hivyo..


Usinione bweg baba(Karubandika aaa),usinione bweg baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....

(Nguza); Nilitaka kujitumbukiza ndani ya moto mie,kumbe bwana yule hana kitanda wala shuka,pa kulala hana analala kwenye stendi ya basi,pa kulala hana anakesha kwenye kituo cha City,Karubandika yoyo,acha vituko we baba....

Usinione bweg baba(Karubandika aaa),usinione bweg baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....
Usinione bweg baba,usinione bwegbaba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....


Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment