Willium Waziri Mkurugenzi,
Willumu Waziri Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Ludewa,
Na Barnabas njenjema
Ludewa
, siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa wabunge, madiwani na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kufanyika hapa nchini Tanzania Mkurungezi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa ambae ni Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ludewa Bw, Willium Waziri amewataka mawakala wa vyama vya Siasa kushiriki kikamilifu na kwa uaminifu zoezi la uchaguzi na hatimaye kutoa majibu ya kweli kwa wananchi wilayani Hapa.
Alitoa maagizo hayo mapema hii leo wakati akifanya mazungumzo na www.maikoluoga.blogsport.com Ofisini Kwake Ludewa na kusema kuwa kunabaadhi ya wahusika wanatakiwa kupatikana muda wote kituoni kuanzia mwanzo hadi mwisho wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema jumapili hii.
Aliwataja wahusika hao ambao wanatakiwa kupatikana vituoni kuwa ni pamoja na Msimamizi wa kituo, Msimamizi msaidizi wa kituo, Mawakala wa upigaji kura kutoka vyama vinavyoshiriki mchakato wa Uchaguzi, Wapigakura wenyewe, msaidizi wa mtu au watu wasiojiweza mfano anaye msindikiza mtu asiye jua kusoma na kuandika pamoja na mtazamaji wa uchaguzi aliyeruhusiwa na tume ya taifa ya Uchaguzi na watu wa mwisho ni Mjumbe wa tume ya taifa ya Uchaguzi Ambae niyeye mkurugenzi kama msimamizi wa Uchaguzi, Askari polisi pamoja na Afisa watume atakaye taka kujua mchakato unavyoendelea.
Aliongeza kuwa hadi sasa maandalizi ya Uchaguzi kwa jimbo la Ludewa yamekamilika ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo shirikishi kwa wasimamizi wa uchaguzi vituoni mafunzo ambayo yalianza rasmi hapo jana na yatakamilika hii leo hatimaye siku ya kesho october 24 wasimamizi hao watasambazwa vituoni tayari kwa kuanza kazi ya usimamizi huo wa uchaguzi siku ya Jumapili october 25 mwaka huu,
Alitoa agizo kwa wanachama wa vyama vya siasa siku ya kukushiriki mchakato wa uchaguzi na baada ya hapo kuwa wavumilivu kusubiri matokeo husika kuwa nani mshindi na mara baada ya kupiga kura waondoke vituoni kwa lengo la kupisha shughuli nyingine za mchakato wa uchaguzi ziweze kuendelea.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo alitoa maelezo kwa wananchi juu ya kutishia kususia uchaguzi wa jumapili kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Ludewa na aliyekuwa akitetea kiti hicho kupitia chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Ludewa kuwa Msiba upokelewe kama kawaida lakini suala la uchaguzi ni muhimu hivyo ni lazima kila mmoja ajitokeze kwenda kupigakura ili kuwachagua Madiwani na Rais huku wakisubiri tamko kutoka tume ya taifa ya uchaguzi juu ya Kufanyika kwa uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo Ludewa kufuatia kifo hicho cha mgombea wa ccm Deo Filikunjombe.
Alisema kuwa yeye kama msimamizi wa uchaguzi ametoa taarifa Ofisi ya Tume ya taifa ya uchaguzi juu ya kifo hicho huku akisema kuwa Tumeitatoa tamko mda wowote kuanzia sasa juu ya Kuanza upya mchakato wa uchaguzi wa Mbunge katika jimbo la Ludewa hivyo wananchi wasikate tamaa kufuatia kifo hicho kwakuwa hayo ni mapenzi ya mwenyezi mungu.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment