Katika kuhitimisha kampeni za udiwani katika kata ya Luana iliyopo Wilayani Ludewa mkoani Njombe KUMEKUWA na vurugu za aina yake kata hiyo imemaliza kampeni zake kwa vurugu baina ya vyama viwili vyenye upinzani mkali kutoka kwa wafuasi wa chadema pamoja ccm.
Vurugu izo zimetokea katika kijiji cha Mbwila kilichopo katika kata hiyo wakati chadema wakimalizia mkutano katika kijiji hicho ndipo wapovamiwa na chama cha democrasia na maendeleo chadema wakiwa kwenye gari aina ya kenta.
vurugu zilidumu takribani saa moja ndipo walipofika polisi kutoka makao makuu ya jeshi la polisi wilaya ya Ludewa.
mara baada ya kutoa taarifa kwa jeshi la polisi walifika katika kijiji hicho na kukuta hali shwari mara baada ya usuluhishi wa amani kwa viongozi wa vyama vyote viwili vya ccm na chadema.
kwa upande wake mgombea wa udiwani kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo Mr. Wilibard Mwinuka amewaomba wananchi wa kata hiyo kabla ya kwenda kupiga kura ni vyema waende kwanza kusali ili Mungu awaongoze katika kuchagua kiongozi aliye bora.
akijibu tuhuma za mgombea wa udiwani kwa tiketi ya ccm Mr.lugome amesema mgombea huyo hana sifa ya kuwa diwani wa kata hiyo kutokana na kuwa na kashfa za kukutwa na rushwa alipokuwa akifanya kazi huko kyela na alihukumiwa lakini pia alishangaa juu ya elimu ya mgombea huyo kwa tiketi ya ccm.
Mbali ya mambo mengi aliyoyafanya kwa kata hiyo amewaomba wananchi wa kata ya Luana kuchagua kiongozi bora aliyetumwa na Mungu kuwakomboa wananchi wa kata hiyo
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment