Marehemu wawili wakutwa porini Makete, wazikwa hapo hapo kutokana na kuharibika vibaya


 

 Marehemu wawili wakutwa porini Makete, wazikwa hapo hapo kutokana na kuharibika vibaya By Edwin Moshi at Friday, October 16, 2015 Na Henricky Idawa  Watu wawili wa jinsi ya kiume wamekutwa wamefariki dunia katika milima ya Machungio ya mifugo ya kijiji cha Ihela kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe.  Taarifa kutoka eneo la tukio zilizothibitishwa na matendaji wa kijiji cha ihela Bw.Alex Mahenge ni kuwa wamekuta miili ya watu wawili mmoja akiwa na begi na vitambulisho huku mwili mwingine ukikutwa bila vielelezo vyovyote katika milima hiyoinayopakana na kijiji cha ibaga magona kijiji hicho.  Amesema kuwa mmoja ametambuliwa kwa vitambulisho vilivyokutwa kuwa ni Therapion B Komba,mwenye umri miaka 61 mkazi wa kata ya Tanga kijiji cha Mlete huku mwingine akishindikana kutambuliwa kutokana na kutokuwa na vielelezo vyovyote anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 50 hivi..  Amesema kuwa taarifa za uwepo wa miili hiyo ilitoka kwa mmoja wa wachungaji wa ng’ombe aliyekwenda machungioni kutafuta ng’ombe kwa ajili ya kuzirejesha nyumbani ndipo alipokuta miili hiyo jana tarehe 15 oktoba mwaka huu na kuripoti ofisi ya mtendaji wa kijiji hicho majira ya jioni.  Akizungumza shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa aliukuta mwili mmoja pamoja na begi la nguo katika mlima huo na baada ya kuzipata ng’ombe zake aliporudi nyumbani aliripoti kwa mtendaji wa kijiiji na ndipo hii leo tarehe 16 oktoba mwaka huu mapema wameenda eneo la tukio.  Marehemu Komba moja ya tiketi yake imeonesha alisafiri kutoka Njombe kwenda Ikonda tarehe 31 Juni mwaka huu,huku vielelezo vingine vikionesha alikuwa akiumwa na ambaye hajatambuliwa akikutwa na vidonge kwenye soksi.  Miili ya marehemu wote wawili imezikwa milimani huko kutokana na kuaharibika vibaya huku vielelezo vilivyopatikana vikipelekwa kituo cha polisi Tandala kwa ajili ya hatua za kisheria.  Mwandishi wetu bado anaendelea kumtafuta kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe kuzungumzia tukio hilo

Marehemu wawili wakutwa porini Makete, wazikwa hapo hapo kutokana na kuharibika vibaya

Na Henricky Idawa

Watu wawili wa jinsi ya kiume wamekutwa wamefariki dunia katika milima ya Machungio ya mifugo ya kijiji cha Ihela kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe.

Taarifa kutoka eneo la tukio zilizothibitishwa na matendaji wa kijiji cha ihela Bw.Alex Mahenge ni kuwa wamekuta miili ya watu wawili mmoja akiwa na begi na vitambulisho huku mwili mwingine ukikutwa bila vielelezo vyovyote katika milima hiyoinayopakana na kijiji cha ibaga magona kijiji hicho.

Amesema kuwa mmoja ametambuliwa kwa vitambulisho vilivyokutwa kuwa ni Therapion B Komba,mwenye umri miaka 61 mkazi wa kata ya Tanga kijiji cha Mlete huku mwingine akishindikana kutambuliwa kutokana na kutokuwa na vielelezo vyovyote anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 50 hivi..

Amesema kuwa taarifa za uwepo wa miili hiyo ilitoka kwa mmoja wa wachungaji wa ng’ombe aliyekwenda machungioni kutafuta ng’ombe kwa ajili ya kuzirejesha nyumbani ndipo alipokuta miili hiyo jana tarehe 15 oktoba mwaka huu na kuripoti ofisi ya mtendaji wa kijiji hicho majira ya jioni.

Akizungumza shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa aliukuta mwili mmoja pamoja na begi la nguo katika mlima huo na baada ya kuzipata ng’ombe zake aliporudi nyumbani aliripoti kwa mtendaji wa kijiiji na ndipo hii leo tarehe 16 oktoba mwaka huu mapema wameenda eneo la tukio.

Marehemu Komba moja ya tiketi yake imeonesha alisafiri kutoka Njombe kwenda Ikonda tarehe 31 Juni mwaka huu,huku vielelezo vingine vikionesha alikuwa akiumwa na ambaye hajatambuliwa akikutwa na vidonge kwenye soksi.

Miili ya marehemu wote wawili imezikwa milimani huko kutokana na kuaharibika vibaya huku vielelezo vilivyopatikana vikipelekwa kituo cha polisi Tandala kwa ajili ya hatua za kisheria.

Mwandishi wetu bado anaendelea kumtafuta kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe kuzungumzia tukio hilo
- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/10/marehemu-wawili-wakutwa-porini-makete.html#sthash.66NrhhEe.dpuf

Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: