ILI KUMALIZA 4 BORA MSIMU HUU, CHELSEA INAPASWA KUVUNJA REKOD



MOURINHO-TAABANIBAADA ya kuanza vibaya Msimu huu, Chelsea wanapaswa kuweka Historia ikiwa watataka kumaliza kwenye 4 Bora za Ligi Kuu England.
Chelsea, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Ligi hii, wapo Nafasi ya 15 wakiwa na Pointi 11 kwa Mechi 10 hadi sasa.
Katika Historia ya Ligi Kuu England, hakuna Timu iliyokuwa na chini ya Pointi 13BPL-STAND-OCT30 kwenye hatua hii ikaweza kumaliza ndani ya 4 Bora mwishoni mwa Msimu.
Ni Timu 2 tu ambazo zilikuwa na Pointi 13 baada ya Mechi 10 kuweza kumaliza 4 Bora na hizo ni Leeds United, ambao kwenye Msimu wa 1998/99 walikuwa na Pointi 13 baada ya Mechi 10 na kumaliza Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 67, na nyingine ni Man United, chini ya Louis van Gaal Msimu uliopita waliomaliza Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 70.
Hali hii inafanya kibarua cha Chelsea kuwa kigumu huku kutetea Ubingwa wao kukionekana kuwa ndoto tu kwani Timu pekee iliyowahi kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England ikiwa na Pointi chache kwenye hatua hii ni Man United ilipokuwa na Pointi 18 kwenye Misimu ya 1992/93 na 2002/03.
Wikiendi hii, Chelsea ina kibarua kigumu ikipambana na Liverpool chini ya Jurgen Klopp.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 31
1545 Chelsea v Liverpool  
1800 Crystal Palace v Man United         
1800 Man City v Norwich           
1800 Newcastle v Stoke             
1800 Swansea v Arsenal             
1800 Watford v West Ham         
1800 West Brom v Leicester                 
Jumapili Novemba 1
1630 Everton v Sunderland                  
1900 Southampton v Bournemouth                 
Jumatatu Novemba 2
2300 Tottenham v Aston Villa      


Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: