SECONDARY SCHOOL sehemu ya 16






















SECONDARY SCHOOL

Sehemu Ya 16

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Ilipoishia Jana →↓↓

"aaaaaaaa sasa utaaribu we vunga kama wiki mbili hivi afu mwambie mimba imetoka"
"sitaki kumdanganya tena mwanamke mwenzangu"
"kwaio sasa na mimi sitaki"
"basi nampigia simu"
"simu ipi? simu yako si hii hapa ninayo"
"namba yake naijua kichwani"
"ivi sesi mbona una gubu sana we mwanamke Eee? au tayari keshakunogesha na hizo ahadi alizokupa?"
"nimeshasema boss mi nataka mimba kutoka kwako"

SONGA NAYOOOO



Nilikua kama sielewi chochote kile coz sesi keshanogeshwa na ahadi alizopewa na kujisahau utu wake, Lakini mtoto wa kiume nilikaza hivyo hivyo na wala sikua wakupaparika. Kwani kutia mimba naweza, tena mimi mwenyewe ndio najijua urijali wangu ila sema malezi niliolelewa ni malezi makali mno. yaani nimelelewa katika malezi ya kidini, Hivyo tendo la kufanya mapenzi kwangu naona kama haramu kubwa sana katika maisha yangu, na nilishasemaga kua sitokaa kuja kusex hata siku moja.

Sasa sesi alikua anaumiza kichwa kwa kupata mimba coz hawezi kubeba mimba tofaut na mimi kwasababu ikija kugundulika kua haikua mimba yangu... heeee sesi atakiona cha mtema kuni, hivyo sesi anaomba sana kwa mungu ili nikubali kumpa mimba ili hizo ahadi alizo ahidiwa azipate,
"boss? sasa unanifikiriaje?"
"kuusu nini?"
Nilikua zangu bize naendelea kusaini mikataba mbali mbali ya kampuni zinazotaka kuweka tawi katika kampuni yetu....
"nataka mimba"
"siwezi"
"kivipi sasa?"
"sesi? hebu naomba unieshim sawa? mimi ni tofauti na huyo boss wako unaemtegemea sawa? kwahio nakuomba sana niache nifanye kazi"
Sesi alikua kama haelewi kinacho endelea Yaani alikua hataki kuelewa hicho ninachokiongea.
"boss? mimi nitampigia simu kua hukufanya na mimi chochote"
"lakini sesi? mbona mijidume ipo mngi tu? si uende ikakupe mimba huko"
"nimesema nakutaka wewe. na niko tayari kuipokea mimba hio"
"ivi sesi? nifanye nini ili unielewe?"
"uni..uni...uniiingizie hio nanii yako"
"sasa skia.. mimi nitakupa mara mbili ya hivyo ulivyoahidiwa na huyo boss wako"
"kivipi?"
"vyote alivyokuaidi kua ukipata mimba atakupa vx mayai... sasa mimi nakupa vx mbili na milioni 10 juu"
"acha utani boss?"
"kweli nakuambia ila ujue tu jinsi ya kumdanganya huyo boss wako"
"lini sasa utanipa?"
"hata kesho ukita nakupa"

USIYARUKE HAYO MAANDISHI HAPO CHINI→→↓↓↓↓↓

NDUGU MSOMAJI WA STORI HIII... MIMI NILISHASEMA KUA SISI NI MATAJIRI WA HASWA...... YAANI KWA HAPA TANZANIA LABDA UTULINGANISHE NA BAKHRESA. LABDA NDIO UTAWEZA KUJUA UTAJIRI WETU ULIVYO. HIVYO USISHANGAE KUONA MIMI MTOTO NAWEZA KUTOA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 50 KWA SIKU,.... COZ HATA MTOTO WA BAKHRESA HAWEZI KOSA HATA MILIONI 100 AU NA ZAIDI KWENYE AKAUNTI YAKE HUKO BENKI..... HIVYO MIMI MWENYEWE KILA WIKI NAWEKEWA MILIONI MOJA KWENYE AKAUNTI YANGU NA WAZAZI WANGU.. KWA AJILI YA KUNUNUA VITU VIDOGO VIDOGO AMBAVYO SIO LAZIMA NIWAELEZE WAZAZI... JAPO HATA KAMA NIKIELEZEA WATANUNUA. ILA WAMENIFUNGULIA AKAUNTI YA BENKI KWA AJILI YA VITU VIDOGO VIDOGO NINAVYOVIPENDA MIMI... SASA IMAGEN TOKA NAANZA SHULE YA MSINGI MPAKA LEO SECONDARY SCHOOL JE? NITAKUA NA PESA NGAPI KWENYE AKAUNTI YANGU? NA JE? NITASHINDWA KUNUNUA HATA GARI MBILI ZA KUMTULIZA HUYU BWEGE??? ACHA UTANI WEWE... WACHA NIHONGE MIEEE

Sasa mtoto alizima fegi kuskia hata kesho naweza kumpa hizo pesa na gari,
Basi kwa sababu hio mtoto aliniinamia na kunibusu kwenye paji la uso kwa furaha.... Sasa ndio nikajiuliza kua,
"kumbe alikua anapenda kubeba mimba kisa ni utajiri weeeetuuu sasa nimeeelewa.. na tena naarisha kumpa hivyo vitu"
Mara kama kanistukia kuna kitu nilikua nawaza kwa muda huo. Hivyo akaniuliza kwa furaha kubwaaa
"mbona umebadirika ghafla boss?"
"wala tu ila nimeairisha kukupa hivyo vitu"
"Whatt?????"
"Whati unasoma unaandika?"
"nakusemea kwa mama ako hukusex na mimi"
"waaaaiiiii kaseme kwani itadhuru nini?? tena itakudhuru wewe mwenyewe"
"kivipi?"
"si umeshaanza kumdanganya boss wako kua umesex na mimi"
"mungu wangu boss nisamee basi na naomba ushauri basi"
"Ebu niachie mimi...afu muda wa kwenda nyumbani umefika toka nje?!
"bossiiii"
"nimesema toka njeeeeee?"
Sesi alitoka lakini alikua analia kwa kumtolea nje kwa kila kitu....

Kweli ulifika muda wa kuondoka na kwenda nyumbani. kwani ilikua ni saa 11:15 jioni... sikua na cha kubeba hivyo nilitoka mikono tupu kisha nikafunga ofisi ya boss vizuri na ufu nikatoka na ufunguo.....
"sesi? we sesi?"
Sesi nilikua namuita lakini alikua haitiki kabisa...
"ok ashura?"
"abeee boss?"
"kevin yuko wapi?"
"yupo toilet boss"
"ok akija mwambie....aaaa basi huyo anakuja mwenyewe"
"aaaa boss?"
"sema kevin?"
"saaafi tu...na tunashukuru kwa kutuandalia kasherehe ketu"
"hahahaha kawaida tu...ok sasa? hebu hakikisha watu wote wametoka then funga ofisi sawa?"
"ok sawa boss. naaa kule ofisini kwako umefunga?"
"yes nimefunga na ufunguo ninao"
"ok haina shida boss we kapumzike tu sisi tutafunga"
"sawa"
Basi nilichukua BMX yangu na kutoka zangu.... wafanya kazi wananishangaa kwa kuona naendesha baiskeli badala ya gari
Nilitoka zangu pale huku nikiwa na mawazo juu ya sesi kutaka ujauzito kutoka kwangu. Nilikua naumiza kichwa sana tu huku nikiendesha baiskeli yangu...

Hua sinaga pakupitia tofauti na msikitini. Hivyo niliingia zangu masjidi na kuanza kusali swala zilizonipita kuanzia mchana. maana swala ya asubuhi niliiswalia nyumbani, japo haiswiii kwa mwanaume kuswalia nyumbani kama mwanamke. Basi nililipia baadhi ya swala kisha nikachukua mswaafu wa hapo masjidi na kuupitia kidogo. Nikicheki muda inaelekea ni saa 12 kasoro. Niliona ngoja niende nyumbani nikaoge kisha nje kuswali swala ya saa 12 jioni.

Nilitoka pale masjidi taaratibu kabisa huku nikiimba nyimbo zangu za kiislamu...
Sasa nilipofika nyumbani kwa nje ya geti Nilishangaa kusikia mziki nyumbani kwetu.... Nikagonga geti kisha mlinzi akafungua. kabla sijaingia nikamuuliza mlinzi
"asee kuna nini uko tena?"
"kuna sherehe"
"heeeeee ya nani tena? coz hakuna mtu aliezaliwa mwezi huu ndani kwetu"
"kwa mimi naona hiii sherehe inakuusu wewe"
"kivipi?"
"sijui ila we ingia tu"
"mh mh apana mi siingiii"
Nikafungua kadirisha cha mlinzi kile ambacho kipo kwenye geti kwaajili ya mlinzi kumchungulia anaegonga. Sasa nikawa nachungulia ili nione hio sherehe yenyewe ipoje ipoje....
Mara anti mwaju kaniona. Akaja mpaka nje huku akiwa na yeye kapendeza ile mvaya

"we sheby mbona upo nje?"
"ah mi sielewi kupoje huko ndani"
"jamani mwanangu hio ni sherehe yako"
"sherehe yangu ya nini sasa?"
"mi mwenyewe sijui"
"kivipi lakini ant?"
"mimi nilishangaa marafiki wa mama yako wamekuja na marafiki wa dada yako zai"
"sawa sikatai ila nataka nijue sababu ya hii sherehe"
"kiukweli sijui.... ila we ingia tu"
"hapana anti mi siingii"
"hapana sheby nakuomba ingia.... kwasababu utamueibisha mama ako"
"bora aeibike tu kuliko kufanya sherehe pasipo watu wengine kujua"
"hapana mimi sikukubalii kabisa, kwasababu hapo walipo wanakusubiria wewe tu"
"sitaki kwakweli bora waende hao wageni"
"sheby?"
"naam anti?"
"heshma imeshuka si ndio?"
"kivipi anti?"
"naona umeshindwa kueshim wito wangu si ndio?"
"lakini anti?"
"lakini nini? sasa mi nasema ingia ndani"
"antiiiii"
"iiingiaaa ndaaanii?"
"sawa basi naingia"
Daaahhh anti alinilazimisha kuingia ndani huku nikiwa sijapenda kushereheka na hio sherehe yao. Niliingia na kushangaa mama angu kanikimbilia huku akisema
"sapraaaaaizi my baby boy"
Tukakumbatiana kwa furaha huku nikijichekesha kinafiki nafiki.
"mamaa?"
"nini mwanangu?"
"sherehe ya nini sasa?"
"mwanangu mi nimefurahi tu kwa leo sasa kwanini nisifurahi na watoto wangu?"
"lakini mamaa?"
"hebu acha maswali yako mwanangu njoo utukatie keki hapa"
Ilibidi tu nimueshim mama angu, hivyo nilifika pale katikati na kuanza kutambulishwa kwa wageni waliokuja
"jamani mabibi na mabwana, huyu ndio kijana niliowaambia mwanzi, na huyu ndio last born wangu... nampenda sana"
Watu waligonga cheazi kwa furaha ya kunifahamu mimi. Sasa mama akaniambia nizunguke nimsalimie kila mtu daahhh. Nikaona nikikataa itakua sio heshma nzuri... Hivyo nikaanza kuwasalimia wote kwa kuwapa mkono. ila cha ajabu wengine walikua wakinitekenya kwwnye mkono afu nikimuangalia ananikonyeza.... Mmhhhh nilishindwa kuelewa kinachoendelea.

Baada ya masaa kadhaa kupita sherehe ilikua imekwisha. sasa mama alikua kawasindikiza marafiki zake kwa kutumia gari...
Sasa nilipomuona zai nikamfuata na kumshika mkono huku nikimburuza mpaka geto kwangu huku nikiwa na hasira hio duuu...
Nilimfikisha hadi geto kisha nikambwaga kitandani kwangu kisha nikaanza kuvua mkanda wangu
"heee sheby? unataka kunifanya nini sheby?"
"tuliaaa, nyie si mnaniona mi hanisi si ndio?"
"sheby una nini wewe? hebu kumbuka mi ni dada yako sheby"

ITAENDELEAAA
usikose kesho mda huu huu


Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: