Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeendelea leo October 20 kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya. Miongoni mwa mchezo uliyovuta hisia za mashabiki wengi wa soka ni mchezo kati ya Arsenal dhidi ya FC Bayern Munich ya Ujerumani ambayo kabla ya mchezo huo kumalizika ilikuwa haijapoteza mechi hata moja.
Kikubwa kilichokuwa ni kivutio cha mechi hiyo ni mashabiki wa soka walitaka kuona kama Arsenal ingevunja rekodi yake yenyewe, Arsenal
ambayo ilikuwa imeshapoteza michezo miwili ya awali, ilikuwa haijawahi
kupoteza mechi tatu mfululizo za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Klabu ya Arsenal ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani imeibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya FC Bayern Munich.
Mchezo ambao ulikuwa hukichezwa kwa
tahadhari kwa timu zote hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika kulikuwa
hakuna timu iliyokuwa imeona nyavu za mwenzake. Arsenal
ambayo ilikuwa na wakati mgumu wa kutaka kufufua matumaini ya kutaka
kufuzu hatua ya 16 ilianza kupachika goli dakika ya 77 kupitia kwa Olivier Giroud kabla ya dakika ya 90 Mesut Ozil kuhitimisha kwa kufunga goli la pili.
Video ya Magoli ya Arsenal Vs FC Bayern Munich
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment