Wakala wa Raheem Sterling ametaja kosa alilolifanya Brendan Rodgers hadi Raheem Sterling akahama Liverpol




Bado zile stori za Raheem Sterling kuhama Liverpool na kujiunga na Manchester City pamoja na kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Brendan Rodgers zinazidi kuchukua headlines. Wakala wa winga huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye asili ya Jamaica Aidy Ward amefunguka na kueleza kuwa aliyesababisha Raheem Sterling ahame Liverpool ni Brendan Rodgers.
“Raheem angeweza kubakia Liverpool, nafikiri kwangu mimi nilikuwa nimeshazungumza na Raheem na angesaini mkataba mpya, mwezi December nilizungumza na Liverpool kuhusu Raheem kusaini mkataba mpya kama tu vipengele vya mkataba wake vingewekwa wazi kama mikataba mingine ilivyo” >>> Aidy Ward
Football-370376
“Lakini katika mkutano na waandishi wa habari Rodgers alithibitisha kuwa Raheem atasaini licha ya kuwa hatukuwa tumefikia makubaliano yoyote, kwa nini alifanya vile? nilijua Rodgers na Liverpool walikuwa wanajua kinachoendelea, lakini kwa sasa angeweza kuwa mchezaji wa Liverpool lakini yupo Man City ni sehemu nzuri kwake”>>> Aidy Ward
Kuondoka kwa Raheem Sterling ndani ya Liverpool kuliweka headlines nyingi katika vyombo vya habari vya Uingereza hususani ukilinganisha na dau la usajili la pound milioni 49 walilotoa Man City ili wapate saini ya nyota huyo kinda wa kiingereza.

Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: