Yanga ndiyo kinara kwa kupata ushindi mara nyingi zaidi ya Simba tangu kuanza kwa Ligi ya soka Tanzania bara


JUMAMOSI ya Septemba 26 moto utawaka uwanja wa taifa Dar es Salaam wakati miamba ya soka Tanzania klabu za Yanga na Simba zitakapomenyana kuwania pointi tatu muhimu ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa nne wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania mara msimu wa 2015/16.
Timu hizo mbili zimekuwa na upinzani mkubwa tangu zilipoanzishwa miaka ya 1935 na 1936,kitu ambacho kimechangia kuwepo uhasama mkubwa na kusababisha kugawana bara bara.

Ushindi

Yanga ndiyo kinara kwa kupata ushindi mara nyingi zaidi ya Simba tangu kuanza kwa Ligi ya soka Tanzania bara wakati huo ikiitwa Daraja la kwanza na sasa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Ubingwa 
Takwimu za mafanikio zinaonyesha Yanga ndiyo timu inayoongoza kwa kutwaa ubingwa wa Tanzania mara nyingi zaidi ya timu zote 15 zinazo shiriki Ligi ya msimu huu ambapo imeweza kubeba ubingwa huo mara 25 huku mpinzani wake Simba ikifanya hivyo mara 18, na klabu za Mtibwa Sugar na Coastal Union ya Tanga zikifuatia.



Magoli - Unazikumba zile 6 za Simba?


Rekodi pekee ambayo ni nzuri kwa Simba katika mapambano yake na Yanga ni kupata ushindi wa mabao 6-0, katika mechi ya Ligi daraja la kwanza Tanzania bara 1977 na ikapata matokeo mengine ya ushindi mnono Mei 6 mwaka 2012 ilipoifunga Yanga mabao 5-0,uwanja wa taifa Dar es Salaam.

Simba imekuwa makini kwa kutumia vizuri madhaifu yawapinzani wao inapo wakuta wamechoka na kufunga mabao mengi yanayowapa rekodi nzuri kwenye historia za timu hizo.

Mechi ya mwisho 
Simba inaingia kwenye mchezo wa Jumamosi ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 1-0, ilioupata kwenye mchezo wa mzunguko wa mwisho bao lililofungwa na Emmanuel Okwi, ambaye hatokuwepo kwenye mchezo huo baada ya kuuzwa nchini Denmark.

Michezo 6 iliyopita
Takwimu za Goal za zinaonyesha Katika michezo 6 ya mwisho ya timu hizo kukutana katika ligi kuu, kila timu imefanikiwa kushinda mara moja huku mechi nne zikimalizika kwa sare.
Katika michezo ya msimu wa 2012/13, gemu ya mzunguko wa kwanza ilimalizika kwa sare ya kufungana 1-1 mwezi Oktoba, 2012, Yanga wakisawazisha dakika za mwisho kwa mkwaju wa penalti uliofungwa na Said Bahanuzi.
Katika mchezo wa mzunguko wa pili Yanga ilishinda mabao 2-0, mabao ya Didier Kavumbagu na Hamisi Kiiza ambao kwa sasa wote hawapo Kiiza akihamia upande wa pili Simba mwezi Mei, 2013.
Ushindi huo wa Yanga ndio ulikuwa wa mwisho kwa timu hiyo kuwafunga watani zao Simba kwani hata walipokutana nje ya ligi katika mechi za Nani Mtani Jembe, Yanga imeweza kupoteza mechi zote mbili tena kwa idadi kubwa ya mabao.
Ilifungwa 3-1, Disemba, 2013 kisha wakachapwa 2-0, Disemba, 2014. Msimu wa 2013/14, na vipigo hivyo vilipelekea kufukuzwa kwa makocha waliokuwepo kwa wakati huo mara ya mwisho Mbrazili Marcio Maximo alifungashiwa virago vyake.
Timu hizo zilitoka sare katika michezo yote miwili. Suluhu-tasa ya 0-0 ilipatikana katika mchezo wa kwanza mwezi Oktoba, 2013 kisha zikafungana 1-1 katika mchezo wa marejeano April, 2014 Yanga wakisawazisha dakika za mwisho.
Sare ya tatu mfululizo ilipatikana katika mechi ya kwanza ya msimu wa 2014/15. Oktoba, 2014 Simba ikitumia kundi la yosso wa tano kutoka timu yao ya pili na wengine wawili waliokuwa wamesajiliwa msimu uliopita iliwabana Yanga na kulazimisha suluhu-tasa ya 0-0.
Katika mchezo wa marejeano Yanga wakachapwa 1-0 mwezi Machi mwaka huu bao la Emmanuel okwi dakika 7 kabla ya gemu kumalizika. Huo ulikuwa ni ushindi wa kwanza wa Simba dhidi ya Yanga katika ligi kuu Tangu Mei, 2012 waliposhinda 5-0. Je, nani mshindi wa mchezo wa Jumamosi hii Septemba 26?


Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment