Watafiti
wanaoandaliwa kufanya utafiti wa masuala mbalimbali hasa ya kielimu kwa
watoto wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kufanya kazi hiyo kwa
moyo mkunjufu, na si kupika takwimu kwa maana ya kutoa takwimu za uongo
Kauli
hiyo imetolewa leo na Afisa elimu Msingi wilaya ya Makete Mwl. Antony
Mpiluka (pichani juu) wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa
watafiti wanaotarajiwa kuendesha zoezi hilo wilayani hapa, mafunzo
yanayotolewa na shirika lisilo la kiserikali la SUMASESU
Mpiluka
amesema kutoa takwimu za uongo kutapelekea madhara makubwa kwa wilaya
huku akitolea mfano kipengele cha watoto kujua kusoma kiswahili na
kiingereza pamoja na kufanya hesabu, kuwa endapo watapika takwimu na
kuonesha watoto wanajua kusoma wote ili hali hawajui, itapelekea wilaya
kuwa na sifa nzuri lakini ni ya uongo
Mafunzo hayo ni ya siku mbili na yameshirikisha vijana kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Makete na yataendeshwa kwa siku mbili
Baadhi ya washiriki wakifuatilia
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko