WAGOMBEA wa nafasi za Ubunge na Udiwani katika Wilaya ya Hanang, Manyara wamedai kutokua na imani na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hanang, Felix Mabula ambaye ni Msimamizi mkuu wa uchaguzi katika jimbo hilo. Wagombea hao wamedai hawana imani naye kwa kuwa Mkurugenzi huyo alikumbwa na tuhuma nyingi za matumizi mabaya ya fedha kwenye miradi ya maji na kuboresha miundombinu ya shule za msingi tuhuma ambazo
zinazowapa hofu haki kutotendeka chini ya msimamizi huyo. Mgombea Ubunge katika jimbo la Hanang kwa tiketi ya Chadema, Derick Magoma amesema tayari wameandikia barua tume ya Uchaguzi yenye kumbukumbu namba CDM/HAN/UT/2/239 juu ya kutokua na imani na msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo barua waliyoiwasilisha Septemba 2 mwaka huu na kuitaka Tume iteue msimamizi mwingine. Magoma amesema kuwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zilijadiliwa katika Baraza la Madiwani zikiongozwa na madiwani wa CHADEMA ambao ni Ndugu Peter Lori Diwani wa Kata ya Katesh, John Farayo diwani kata ya Endasiwold, Masala Bajuta wa kata ya Gisambalang na wengine. “Madiwani hao waliomtuhumu Mabula ndio wagombea na hao hao Mabula atasimamia uchaguzi wao, tunaona kabisa kuwa haki haiwezi kutendeka na hata kama ikitendeka hatutaamini kama imetendeka,” Amesema Magoma Mgombea huyo amesema kuwa Mabula anakabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya Sh. 1.1 bilioni ambazo zimepotea na zingetumika kujenga vituo vya afya, kuleta madawa na kusambaza huduma ya maji safi ambayo ni changamoto kubwa kwa jimbo hilo. Mgombea udiwani kata ya Endasiwold, John Farayo amesema kuwa wao kama wagombea hawana imani na Mkurugenzi huyo hivyo wameitaka tume ya uchaguzi ichukue hatua za haraka kumteua msimamizi mwingine wa uchaguzi ili uchaguzi uwe huru na wa haki. Mwenyekiti wa Chadema Hanan`g, Isack Joseph amesema kuwa chama hicho kimesimamisha wagombea udiwani 31 kati ya kata 33 na kufafanua kuwa kutokana na rekodi ya Mkurugenzi huyo wanahitaji msimamizi mwingine wa uchaguzi ambaye watakua na imani naye. Na Ferdinand Shayo, Hanang
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment