SECONDARY SCHOOL
Sehemu Ya 7
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Ilipoishia Jana →↓↓
"we zai hio chupi ni ya nani na umeitoa wapi?"
Aliulizwa na mama kusiana na hio chupi aliokua akimuonyesha mama.. na ilikua ni chupi ya kike
"mama hii chupi niliikuta kwenye gari yangu. na sheby jana ndio alikua nalo hili gari kule kwenye msiba wa mwalimu wao"
Nilitoa macho hayo huku nikiwa na hasira hizo duuu
"we sheby mwanangu hii chupi uliitoa wapi?"
SONGA NAYO
"mamaa mi sijui kuusu hio chupi kwani ndio kwanza naiona hapa"
Nilianza kua na kigugumizi cha hapa na pale kwasababu sijui hio chupi ilifikaje huko kwenye gari, kiukweli sikua na jibu la kutoa kuusiana na hio chupi, maana sikumbuki kitu chocho kusu hilo. Kiukweli nilijisikia vibaya sana ila Basi kutokana na kutokua na jibu sahihi basi na kesi iliishia pale pale na chupi ikatupwa...
"we zai huendi harusini?"
Aliulizwa na dada nusura kua haendi
"nitaenda ngojeni nioge kwanza"
"sheby msubiri dada ako mi wacha nitangulie coz mimi ndio mpambe wa bibu harusi"
"aaahh hili litachelewa bwana"
"wala tu hachelewi sawa mdogo wangu?"
"aaa nitamsubiri tu kwa heshima yako"
Basi dada nusura alipanda gari yake na kuondoka, sasa mimi tena nikawa namsubiri zai ili twende wote huko harusini. na kadi ya kuingilia tunayo maana harusi za kitajiri bila kadi ya mwaliko huingiii ng'oo
Ilimchukua kama robo saa hivi hadi kumaliza kuoga Kisha akaenda kujibararua na mavipodozi yake, Kama unavyojua wadada zangu wote ni wazuri na wana maumbo ya maana, afu pia ni mashombe shombe kasoro mimi tu ndio sina asili hio.
Mama yangu ana asiri ya kiarabu kwani baba yake ambae ni babu yangu ni mtanzania na mama yake ambae ni bibi yangu ni muarabu na yupo afrika kusini. Kwahio mama yangu sio muarabu kabisa na wala sio muafrika bali yupo mixer yaani rangi yange haikubezi upande mmoja bali zimechanganyikana kwahio ukitaka kumjua ni mtanzania utaona mixer ya rangi ya ngozi. na ukitaka kujua ni shombe la kiarabu utaona unywele tu. sasa imagen mixer kama hio je? itatotoa watoto wa dizaini gani?.... we acha tu dada zangu ni shida yaani kama ningelikua ni muhuni muhuni duuuu ningesha watamani kitambo sana. ila nashukuru kwa malezi niliopewa ya kumueshimu kila mtu, kuto kumdharau mtu Eti kisa tuna pesa kutamani mapenzi ingali bado ni mdogo na pia dini yetu ya kiislam hairuhusu vitu kama hivyo,
Baada ya muda dada zai alitoka akiwa kavaa kiajabu mmhhh
"sasa ni nguo gani hio umevaa?"
"kwani we unajua nini wewe?"
"aahaaa kwaio mi sijui kitu ee? sawa"
"sasa unaenda wapi?"
"sipandi na wewe gari moja"
"sasa sheby ndio nini hivyo jamani?"
"nimekwambia hivi naenda kupanda dala dala"
Sasa nikiwa ndio naelekea zangu kupanda gari la abiria wengine tofauti na la zai. niliitwa na anti mwaju
"we pumbavu? rudi hapa haraka"
"lakini anti si unamuona zai hio nguo alioivaa jamani"
"nimesema rudi haraka"
"sawa tuuu ila basi akatishie hata kanga tu"
Anti mwaju alivua kanga yake na kumpatia zai
"shika na wewe hebu jizungushie ili ufiche hicho kinguo chako"
Zai alikubali lakini ni kishingo upande
"Eeee bora hivyo sasa Kuliko utembee na shekhe mzima na kimini sketi"
Basi niliingia kwenye gari na dereva ni yeye mwenyewe,
Dada yangu zai ana umbo la kipekee sana kwasababu hata akivaa gunia lakini bado ataonekana tu. sasa hapa alikua kavaa kamini sketi tena kenyewe ni kepesiii afu alikua na chupi tu afu na hio mipaja yake sasa yote ipo nje.. sasa imagen kitu kama hicho je humo ndani ya gari mi si ningeteseka.
Tukiwa safarini zai alionekana kukasirika sana kwa kutopewa uhuru wa kuvaa kiguo chake hicho.
"sasa zai? unanunishwa na nini?"
"niache"
"asa usiambiwe ukweli?"
Wakati huo bado tupo safarini tukielekea kwenye harusi huko kijenge.
"ila sheby hebu ngoja nikuulize swali"
"swali gani hilo?"
"afu mbona anti mwaju anakufokea vile mara akutukane, ivi anajua thamani yako kweli? na aaangesikiwa na mama vile alivyokutukana heeee angefukuzwa kazi siku hio hio hata kama ni wa muda mrefu"
"unajua wewe hukulelewa katika maadili mema na ndio maana hata lile neno pumbavu kwako limekua kama kifo yani?"
"ila anti kazidi kukufokea"
"we muache tu bwana mbona una gubu we zai? ntashuka kwenye mgari wako huuu wewe ooohoo we haya"
"mmhhh basi yaishe"
Basi tulikua kama tunakaribia katika hio harusi husika.
"ila kaka sheby we ni noma kweli yani"
"noma wa nini tena?"
"hehehehehe yaani umenipigia mtu mpaka kaacha chupi duuu kweli kaka yangu we ni noma"
"sikia zai usitake tugombane kabisaa.... kwasababu huezi ukaleta jichupi lako afu ukanisingizia mimi nilikua na mwanamke ndani ya gari"
"we sheby ivi unajua ile chupi sijaitupa bado, sasa hebu ione hii hapa je? mi naweza kuvaa kichupi kidogo hivi?"
"asa mi ntajuaje na mwili wako? kwani mi ni mumeo? afu tueshimiane zai"
"najua ukweli unauma bali mimi sina chupi kama hii afu isitoshe hii chupi ni ndogo kwangu"
"je? kama uliichukua kwa wafanya kazi ili uje unisingizie je?"
"kwanza sinaga mazoea na hao wajinga wajinga"
"ebu lete hio chupi apa"
Niliishika ile chupi kisha nikaitupa huko nje, na wakati huo gari ilikua ikitembea kwa kasi, hivyo kuipata tena ni ngumu
"sasa umeitupia nini jamani?"
"hahahahaha ndio maana nakuambia hio chupi ni yako afu unanibishia"
"lione vile na ule mkichwa wake"
"afu zai unanizoea ee?"
"yaishe Eee?"
Basi tulifika kwenye harusi ambapo kulikua na shangwe nyingi za kusisimua na kila aina ya burudani kasoro kaswida tu ndio sioni.
"aaahh sasa hapa pana maana gani kama hata kaswida sioni?"
"kaswida za nini na wewe?"
"aahh kaswida muimu bwana"
"ebu twende uko.. maana wewe ni wa kushikwa mkono"
"niachie bana zai"
"weeee twende je? ukipotea huku nitamuambiaje mama?"
"si unamuambia tu nimepotea"
"hebu twende"
"subiri sasa mbona unanivuta tuu?"
Basi tulikua tunaelekea kwenye viti maalumu kama V.I.P kisha tukaketi na kuletewa vinywaji aina ya pombe pombe fulani hivi..... Ila mimi nilichagua redbull isio na kilevi chochote,
"nisubiri hapo hapo nakuja"
"unaenda wapi we zai?"
"nakuja bwana na wewe"
Dada zai aliondoka kwenye kiti na sijui alikua anaenda wapi, Haikupita muda mara kuna msichana mrembo na ana umbo hilo afu alikua kavaa mini sketi kama ile ya zai... Alipofika alikaa kwenye siti ya zai
"samaani kuna mtu apa"
"usijali sikai sana"
"ok"
Niliendelea kupata redbull yangu taratibu huku nikiangalia shoo za watu wanao waburudisha waalikwa waliokua hapo
"samaani mkaka sjui umekuja na nani?"
"utaniulizaje swali kama hilo wewe?"
"samaani basi kama nimekuuzi"
"kwanza hujanisalimia afu una miswali ya ajabu ajabu tuu"
"ok mambo vp?"
"waaaiii staki"
"kwanini sasa?"
"nisalimie kidini ndio nitakuitikia"
"haya tumsifu yesu kristo"
"Ati nini? wee mwehu nini yani mi nimtumikie yesu? mwehu kweli wewe"
"sasa matusi yote hayo ni ya nini?"
"sasa utanisalimiaje kiikristo?"
"kwani uliniambia dini yako ni ipi?"
"muislamu"
"ok Asalama Alekhu"
"waalaykha"
"mbona humalizii?"
"kwani we si mkristo?"
"ndio"
"basi ndio sheria yetu kuitikia nusu"
"kwasababu ni mkristo?"
"ndio"
"mmmhhh we muongo wewe"
"basi yaishe afu naomba utoke mwenye hicho kiti atakuja sasa hivi"
"usijali best nitatoka, afu kwani ni nani huyo?"
"unamtakia nini?"
"mbona unaringa we boy"
"kwani nilikuita hapa?"
"basi nisamee"
Nikawa naendelea kucheki tamasha pale jukwaani kabla ya mwali kuletwa.
"ila mkaka we hensamu"
"najijua hivyo sihitaji sifa nyingi"
Nilikua najibu hovyo kwakua tayari nimeshamchoka na maswali yake ya ajabu afu kama vile nimemshtukia vile
Yule dada aliondoka zake baada ya kuona hajibiwi sahihi.
"poa basi bai"
"nenda"
Haikuchukua muda mara zai karudi sasa hapo ndipo nilipojua kua yeye ndie aliemtuma yule dada aje hapa
"vp nimechelewa ee?"
"heeeee ile khanga ya anti mwaju umeeka wapi?"
"ipo huku kwenye kibegi"
"aaahhh kwahio unaona sahihi kutembea na hio mini sket si ndio?"
"afu sheby we unajua ni mdogo kwangu hivyo chunga domo lako ilo"
"haya bwana"
"Eeehee nimeona ulikua na mschana hapa au ndio wifi nini yule?"
"Eeee afu nimemtongoza kanikubalia afu mtoto mzuri ana mwili mzuri kinoma... vp ningependa uanze urafiki nae ili awe anakuja homu"
"haaaaaa unasema kweli sheby?"
"aaaahh chezea mimi wewe"
"mbona yule yule ni rafiki yangu afu hata hivyo mimi ndio nimemwambia hapa aje kwahio nishukuru mimi"
"nyokoooooo lione sasa na hilo lisura lako nininininini nyoooooo heee sijamtongoza wala nini na nilijua tu utakua ulimtuma"
"nani nyoko? sheby nakuuliza nani nyoko?"
Mara kuna mama alitokea pale ila mimi nilikua simjui
"haaaaaa shangazi mamu shkamoo"
Zai anaonekana kumjua mama huyo tena kamuita shangazi mamu.. basi nami nikaita hivyo hivyo kama dada yangu alivyoita
"shkamo shangazi"
"marahaba hujambo?"
"sijambo"
Mara huyo shangazi akaanza kuniangalia usoni huku akimuuliza zai
"zai? mama yako ananiambiaga kua ana kiziwanda wake wa kiume sasa ndio huyu nini?"
"ndio shangazi. huyu ndio last born wetu"
"mmhhh ni hensamu kweli"
Mara shangazi akatoa hela na kumpa zai huku akimwambia kua
"kaninunulie vocha pale"
Sasa kwakua mimi ni mtoto wa kiume na napenda kutumwa hivyo nilitaka kutumwa mimi
"shangazi ngoja niende mimi"
"ah ah muache aende dada yako tu"
Mmhhh nilitulia huku nikiendelea kunya redbull yangu... zai alikua keshaondoka na nikawa nimebaki na shangazi
"ivi shangazi unaitwa nani?"
Yeye ndio aliniuliza.. kwani mtoto wa kiume kuitwa shangazi na shangazi yake sio kesi na pia haina shida... mbaya ni mtu mwingine tofauti na shangazi kumuita mtoto wa kiume shangazi. ila kwa shangazi hua haina shida, Sasa shangazi aliniuliza jina langu nami nilimjibu
"naitwa sharbiny"
"waaoo una jina zuri afu ni hensamu"
"mmhh asante shangazi"
"bwana we sheby usiniite shangazi"
Mmhhh nilishangaa kumsikia shangazi eti nisimuite shangazi
"sasa nikuite nani shangazi"
"naitwa mariamu niite mamu"
"apana shangazi mi sijafunzwa hivyo"
"ok nipe namba yako basi"
"mmh mi sina simu"
"kwanini sheby?"
"nimeamua tu"
"ok sema nikununulie tablet au Iphone 6 au samsung galaxy s4 au unataka gari gani??? niambie basi jamani kabla dada yako hajaja"
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment