SECONDARY SCHOOL
Sehemu Ya 4
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Ilipoishia Jana →↓↓
"fanya fasta mi nataka nikaangalie kaswida"
"mmhhh we nawe unapenda hizo nyimbo zako mbayaaaa"
"afu zai kejeli hua spendi"
"ok yaishe Sasa kuna kitu nataka nikuambie"
"kitu gani hicho?"
"ah ah we kubali kwanza"
"kwani ni kizuri?"
"ndio.. tena ni kizuri saanaaa"
"haya nimekubali"
"sogea sasa nikunong'oneze"
"mbona una masharti hivyo?"
"bwanaaaa sheby we si uje tu"
"haya niambie"
Nikamtegea sikio ili aseme hicho kitu anachotaka kusema
"mwenzio mimi nime.........
SONGA NAYO
Nilikua natega sikio kwa makini sana ili kumsikiliza hicho alichotaka kukiongea. huku akiwa anatabasam zitoooo
"sogea sasa nikunong'oneze"
"mbona una masharti hivyo?"
"bwanaaaa sheby we si uje tu"
"haya niambie"
Nikamtegea sikio ili aseme hicho kitu anachotaka kusema
"mwenzio mimi nimetumwa na jack"
"ushaanza ujinga wako sio?"
"heeee? kwani umeshajua hicho alichonituma?"
"haya kakutuma nini?"
"anaomba kitabu chako"
"heeeee? sasa mimi form 3 na yeye form 4 wapi na wapi?"
"amesema anataka kujikumbushia"
"mmhh poa nikumbushe asubuhi"
Nilitoka zangu kwa hasira maana nilijua kuna cha maana anachotaka kuniambia kumbe ni kuombana vitabu, Mimi na zaituni kiumbo tumelingana ila kiumri kanipita miaka miwili, hivyo tukiwa pamoja unaweza sema ni mapacha wasiofanana. maana tumelingana kiumbo ila yeye ndio mkubwa kiumri, Nilishuka zangu hadi siting rum. nikawa nimekaa na dada yangu nusura, tena nilikua nimemlalia mapajani kwake Yaa kichwa changu kime egemea mapaja yake, hio ni ishara ya upendo kwa ndugu. Tulikua tukipiga stori za hapa na pale
"ivi dada? unaonekana unapenda sana BBA ( Big Brother Africa )"
"ndio tena hii ninayoangalia ni CD tu ila ya mwaka huu lazima niende nikaiwakilishe tz"
"aaaaaaaa mi staki uende buana"
"kwanini nisiende?"
"mmhhh kule wanakaa ovyo sana"
"kivipi?"
"si wakaa bila nguo"
"wai mi siogopi hilo kikubwa nishinde ti"
"haaaaaa kwahio upo tayari mi mdogo wako nikuone?"
"kwani we ni kipi usichokijua?"
"sawaaa navijua vingi ila sio cha dada yangu"
"hehehehehe kumbe unanieshim dada yako eeehh? basi siendi"
"itakua vizuri usipoenda"
Basi nikiwa bado nagala gala katika mapaja ya dada yangu. mara beki tatu ( hausi geli ) kaja pale
"dada chakula tayari"
"sawa tunakuja"
Kwa kawaida nyumba za kitajiri hua zinakua na sebule mbili.. yaani daining room ni sehemu spesho kwa kulia msosi tu. na varandani ni sehemu ya kuangalia tv na kunywa kunywa juice huku stori kwa wingi... Sasa hapo tuliitwa twende tukale msosi,
Nilifika mezani ambako hua sisi watoto wa maboss tunapakuliwa na wafanyakazi. Ila mimi hio tabia sinaga kwani nikifika tu mezani nachukua msaani wangu na mkijiko kisha najipa msosi mwenyewe, Tuliokaa kwenye meza tulikua ni sisi wana familia tu pamoja na anti mwaju. Tulikula pale na madada zangu wakawa wanang'ang'ania kunilisha Eti kisa ni mdogo wao Yani wamemisi kunilisha toka nikiwa mdogo, Nami si unajua nimeshakua ila swaga za kitoto kitoto bado ninazo zile za kitajiri..... kwa maskini saa hizi ningeshaenda kubeba zege uko kwenye masaiti. na utoto ungekua hamna tena... Mara dada nusura akaanza kuongea
"ila mdogo wangu na wewe nunua simu"
Mara zai nae kadakia juu kwa juu
"Eeee mwaya hebu muambie maana nikimuambia mimi anajifanya hasikii"
Nikaona ngoja niwajibu moja la titifotati
"sikia nyie mimi bado nasoma na sihitaji simu aina yeyote Afu we zai fata mambo yako sawa?"
"umeona sheby anavyonijibu eeh?"
Mara mama yangu akaingilia kati
"nyie hebu muacheni kiziwanda wangu, kwani uamuzi wa kuwa na simu ni wake"
"mmhhh mama ila mdogo wetu kazidi yaani utafikiri ni masikini bwana"
Alikua ni dada nusura ndio aliongea hivyo
"afu dada nusura na wewe ushaanza kuniingilia eee?"
"Mmhhh baasi mwaya mdogo wangu nisamee basi"
Zai nae akaongea lake liliozua mjadala kamili
"tatizo ni lile lishule lake analosoma yaani ile shule ina maadili mpaka inakera"
"Ati nini? Mamaa unamsikia mwanao zai anaizarau shule yangu?"
"kwanza hio shule nitakuhamisha muda sio mrefu"
"aaaaaa mamaa sasa ndio mambo gani ayo? mi sihami ile shule"
"ngoja baba ako aje"
"oohooo kwani si nitaongea nae"
"uongee nae nini sasa?"
"si asikubali nihame"
"wakati yeye ndio alilitoa hilo wazo"
"haaaaa jamani mamaa kwani hio shule imewakosea nini?"
"tatizo unatueibisha kwa kusoma shule ya kimasikini kama ile"
"Aaaa Eti anti mwaju kweli unaridhika na jambo hilo kweli?"
"sasa mimi nitafanyaje mwanangu? maana mama yako ndio kasema na mimi sina la kusema"
"duuuu mbona sina mtetezi?. sasa nasema hivi mtafanya mfanyavyo ila shule mi sihami"
Nikatoka pale mezani kwa hasira na kukimbilia chumbani kwangu, Nikachukua vitabu vyangu na kuanza kujisomea... hua mi sinunagi kama watoto wengine wa kitajiri walivyo.. kitu kidogo tu kanuna nuuu... mimi nilikasirika tu kidogo..
Mara ghafla nusura alikuja chumbani kwangu, Na kuwasha tv kisha akakaa kwenye sofa.
"sheby? umechukia kwani?"
"aaahhh mnaanzisha mada zenu za ajabu"
"lakini sio mimi ni dada yako zai ndio kaanzisha"
"aaaahh zima basi hio tv si unaona najisomea?"
"mmhh haya nimeizima"
Sasa alipozima akaja pale kitandani kwangu na kulala kama nilivyolala mimi huku akiangalia ninachokisoma katika kitabu.
"heee ivi haya masomo mshayafikia kwani?"
"Eee tena muda tu"
"mmhh hiki kitabu si cha form 4 hiki?"
"mmhhh"
"ni cha nani?"
"si cha zai"
"kwaio umeshiba?"
"aah sili tena kwani mshaniuzi"
"mmhh na wewe kwani utahamishwa kweli?"
"ahhh mama saa zingine haeleweki huyu"
"mmhh huhami bwana"
"kweli sihami?"
"walikudanganya tu"
Duuuu nilifurahi sana kusikia sihami maana shule yetu ni nzuri na ina maadili mema sasa nikihama na kwenda huko kwenye shule ya kihuni ambayo mwanafunzi anaenda na gari kaliii na simu za bei ghali...
Basi dada yangu alitoka na mimi nikalala zangu, mpaka asubuhi kumekucha ni muda wa kwenda shule.
Nikajiandaa vizuri kisha nikaenda mesani kwa kunywa chai. nilikuta mkate mlaiini uliopakwa kila aina kipakio cha mkate. Duuuuu nilianza kupiga chai huku nikimsifu kimoyo moyo mtu alienitengea chai hii.
Mara Anti mwaju katokea Yule mfanyakazi wetu wa kwanza kabisa ambae hua ndio namuita ANTI MWAJU
"naona unacheka tu peke yako?"
"hehehehehe ndio anti shkamoo?"
"marahaba hujambo?"
"sijambo anti"
"ok ukimaliza utaweka vyombo pale sawa?"
"sawa anti"
Unajua mimi nampenda sana anti mwaju kwasababu hua alinilea katika maadili mema na bado anaendele kunilea hivyo hivyo.... maana hapa kaniambia nitoe vyombo na wakati wafanyakazi wapo tele.,... kwahio hii ni ishara ya malezi mazuri. ila kwa litoto lingine lingeambiwa litoe vyombo... hooooooo angeandamana nyumba nzima.
Basi nilimaliza kula kisha nikawa natoa vyombo huku nikifuta meza. mara beki tatu mmoja kaja
"kaka lete nikuseidie"
"ah ah natoa mwenyewe usijali"
"ah ah bwana ukionekana unatoa wewe nitafokewa"
"usijali nitakutetea tu"
Mara anti mwaju katokea
"we fatu hebu muache atoe mwenyewe. mimi ndio niliomwambia atoe vyombo. kwani akiwa na kwake ataish ishije?"
Basi nilitoa vyombo na kufuta meza kisha nikaingia chumbani kwangu ili nichukue begi kisha nitoke zangu nje nisubiri school bus....
Sasa ile nataka kutoka mara nikakutana uso kwa uso na batuli ambae ni mmoja kati ya mahausi geli wetu.... na hua mahausi geli wetu wote ni wakali na wana maumbo ya mitego ile mbaya...
"nini shida?"
Nilimuuliza kwa kawaida tu
"nimekuja kuchukua nguo nikafue"
"ooohh Ok subiri nikutolee"
Nikaanza kumtolea nguo ambazo nilizivaa ili akafue.
Nilimpa nguo chache tu maana mimi hua sibadiligi kila saa kama mitoto mingine ilivyo na sifa za kutupia mitupio yao....
"kaka mbona ni chache?"
"heeeee sasa nikupe hadi nguo safi nini?"
"boxer huna?"
"heeeeeeee boxer za nini sasa"
"buana kaka mi nataka nikazifue tu"
Je? Nimpe na boxer au nisimpe????
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment