Chama cha Mapinduzi kinapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa.
Mwenendo wa Kampeni
Kwa
kifupi, Mgombea Urais, Ndugu John Pombe Magufuli na Mgombea-Mwenza
Ndugu Samia Suluhu Hassan, wanaendelea vizuri na kampeni. Kila mmoja
anafanya mikutano na wananchi kati ya 8 hadi 11 kwa siku na kukutana na
maelfu kwa maelfu ya wananchi. Tunawashukuru wananchi wanaokuja kwenye
mikutano yetu. Tunawashukuru pia makada wa CCM wanaojitolea kwa hali na
mali kukipigania Chama cha Mapinduzi na kumtafutia kura Ndugu Magufuli.
Tunaridhika
sana na mwenendo wa kampeni yetu. Katika nusu hii ya pili ya kampeni
tutaongeza kasi na msukumo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa mbinu
na mikakati mipya.
Midahalo ya Wagombea
Tumeshangazwa
na kauli ya Ndugu Kajubi Mukajanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari
Tanzania kwamba CCM haijathibitisha kushiriki mdahalo. CCM ilipokea
mwaliko wa MCT na kuijibu kwa barua ya tarehe 13 Septemba 2015 yenye
kumbukumbu CMM/OND/M/190/132 iliyosainiwa na Ndugu Stephen Msami,
Msaidizi wa Katibu Mkuu. Barua hiyo ilipelekwa na kupokelewa kwa
dispatch ambayo nakala yake tunayo. Baada ya hapo, Katibu Mkuu wa CCM,
Ndugu Abdulrahman Kinana, alifanya kikao na wawakilishi wa MCT katika
Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba ili kutaka kujua zaidi na kutoa maoni ya CCM
kuhusu utaratibu mzima wa mdahalo. Katika kikao hicho, ambapo MCT
iliwakilishwa na Afisa wake, Ndugu Allan Lawa, pamoja na Ndugu Tido
Mhando, CCM ilithibitisha tena kushiriki mdahalo. Tatu, tarehe 16
Septemba 2015, CCM ilitoa kauli rasmi, iliyosainiwa, ikithibitisha
kushiriki mdahalo. Kauli ya Ndugu Mukajanga inalenga kuwasaidia kisiasa
wale ambao hawajathibitisha au hawana nia ya kuthibitisha kushiriki. Kwa
msingi huu, tunaamini ni vyema mdahalo huu ukaandaliwa na ushirika wa
taasisi mbalimbali zilizokuwa na nia ya kuandaa midahalo, (kama vile CEO
Roundtable, UDASA, Twaweza) ili kuiondolea uwezo taasisi moja, au
kikundi cha watu wachache, kuhodhi na kuwa na ukiritimba kwenye jambo
hili kubwa na muhimu.
CCM inapenda kusisitiza yafuatayo:
1. Ndugu Magufuli amekubali kushiriki mdahalo wa wagombea Urais
2. Mdahalo uwashirikishe wagombea wenyewe na sio wawakilishi wao.
3. Wagombea wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki.
Tunapozungumzia
mabadiliko katika nchi maana yake ni utayari wa kufanya mambo mapya
yenye tija ambayo hayajawahi kufanyika, ikiwemo mdahalo wa wagombea
Urais. Wanaohubiri mabadiliko huku wakiogopa kushiriki mdahalo
wanahubiri mabadiliko hewa.
Utafiti wa TWAWEZA
CCM
haikushangazwa na matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza
yaliyotangazwa jana ambayo yanatoa ushindi wa asilimia 65 kwa Ndugu John
Pombe Magufuli dhidi ya asilimia 25 za Mgombea wa UKAWA.
Hatukushangazwa na matokeo ya utafiti huu kwasababu tano:
1.
Siku UKAWA walipomteua Ndugu Edward Lowassa kuwa mgombea wao ndio siku
CCM ilipohakikishiwa ushindi katika uchaguzi wa mwaka huu. CCM
hatukumteua kwasababu tuliamini hakuna namna ambapo Watanzania wengi
watamchagua.
2.
Katika uchaguzi wa mwaka huu CCM tunafanya utafiti wetu wa ndani wa
kisanyansi kila wiki kujua mwenendo na mwelekeo wa kampeni na maeneo
yanayohitaji nguvu mahsusi. Tangu tuanze utafiti wetu mwishoni mwa mwezi
Agosti, karibu kila wiki asilimia za ushindi wa CCM hazijawahi kushuka
chini ya asilimia 60 na zimekuwa zinapanda.
3.
Kazi kubwa anayofanya mgombea wetu, Ndugu John Pombe Magufuli, na
mgombea-mwenza, Ndugu Samia Suluhu Hassan, kuzunguka nchi nzima kwa
barabara na kuongea moja kwa moja na wapiga kura inazaa matunda.
Wanawafikia wapiga kura wengi, hasa wa vijijini, na wapiga kura hao
wanawaelewa.
4.
Kampeni kubwa zinazofanywa na wagombea Ubunge na Udiwani wa CCM na
makada na viongozi wa Chama katika ngazi zote nchi nzima kila siku
kumuombea kura Magufuli nazo zinazaa matunda.
5.
Tunaamini pia migogoro ndani ya UKAWA katika kipindi hiki cha uchaguzi
iliyopelekea mitafaruku katika kuachiana majimbo na, baadaye, kutokana
na uteuzi wa Mgombea Urais wa UKAWA, kupelekea kujiuzulu kwa viongozi wa
muda mrefu na maarufu wa UKAWA, Profesa Ibrahim Lipumba na Dr. Wilbrod
Slaa, na migongano ndani ya NCCR-Mageuzi, yote haya yamepunguza imani ya
wananchi kuhusu uwezo wa vyama hivi kushika dola.
Lakini
vilevile matokeo ya utafiti huu ni ishara kwamba Watanzania wamempokea
na kumuelewa Ndugu Magufuli na wako tayari kumkabidhi nchi.
Sisi kama CCM kuna baadhi ya mambo tumeyachukua katika utafiti huu na tutayafanyia kazi ili kujihakikishia ushindi.
Tumeshangazwa
na taharuki, hasa kutoka miongoni mwa wasomi na wanaharakati, kuhusu
matokeo ya utafiti huu. CCM ilitegemea kwamba jamii ya wasomi na
wanaharakati ingefurahia utamaduni wa tafiti za kisiasa unaoanza
kujitokeza hapa nchini ili siku zijazo tujikite katika kurekebishana
kwenye kanuni za utafiti na ithibati na uhakiki wa ubora. Tunasikitika
kwamba yanawekwa mazingira ya kutisha na kukatisha tamaa (atmosphere of
intimidation) kwa watu wanaotaka kufanya tafiti za kisiasa nchini.
Utafiti
ni sayansi. Matokeo ya utafiti hupingwa kwa matokeo ya utafiti
mwingine, sio kwa kuponda tu au kwa matusi na vitisho. Ni vyema
tukajifunza kupokea habari mbaya bila taharuki.
Itakumbukwa
kwamba, mwezi Agosti 2010, taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Synovate
ilitoa utafiti ikionyesha kwamba CCM itashinda Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa
asilimia 61. Baadhi ya wana-CCM hawakufurahishwa na matokeo ya utafiiti
huo kwasababu waliamini kwamba ushindi wetu ulikuwa ni mkubwa zaidi.
Wapinzani waliwalaani, kuwatukana na hata kutaka kuwashtaki Synovate.
Kwenye matokeo halisi ya kura, CCM ilipata asilimia zilezile 61
zilizotabiriwa na Synovate.
Ni vyema kuweka akiba ya maneno kwenye masuala haya.
Imetolewa na:
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
23.09.2015
- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/09/isikupite-taarifa-hii-kutoka-chama-cha.html#sthash.2A5J1iyl.dpufMkutano wa UKAWA na waandishi Wa habari kuhusu utafiti wa TWAWEZA
Umoja
Wa Vyama vinavyounda UKAWA leo wamezungumza na waandishi wa habari
kwenye makao yao makuu yaliyopo maeneo ya Kawe,jijini Dar kuhusu utafiti
uliofanywa hivi karibuni na taasisi ya TWAWEZA kuhusu mwenendo Wa
uchaguzi mkuu hapa nchini.
Akizungumza
kwa niaba ya UKAWA,Mwenyekiti Wa NCCR-Mageuzi,James Mbatia alisema kuwa
taarifa ya taasisi hiyo imeidhalilisha TWAWEZA wenyewe na CCM kwa
ujumla.
"TWAWEZA imejidhalilisha kwa kubagua wagombea urais Wa vyama vingine mbali na CCM na CHADEMA"
"TWAWEZA haifahamu hata idadi ya wagombea ubunge na udiwani,utafiti huo
umetoa ripoti inayokinzana na ukurasa Wa saba,huu utafiti ni Wa uongo"
alisema Mbatia.
"Katika taarifa ya TWAWEZA haijaweza kuhakiki taarifa yake kitakwimu,CCM
imekubaliana na idadi ya watu walioshiriki kwenye utafiti kwa kigezo
cha idadi ya watu 1848"
"CCM hiyo hiyo ilikataa kukubali maoni ya wananchi zaidi ya laki tatu
kwenye rasimu ya katiba ya Warioba,lakini leo wamekubali watu 1848"
aliongeza Mbatia.
"Simu za mkononi na chaja zilizogawiwa ilikuwa ni rushwa iliyotolewa na TWAWEZA kwa washiriki Wa utafiti huo"
"TWAWEZA wanajua vyama vya CUF,NCCR-MAGEUZI,na NLD hawajatoa wagombea
wao Wa urais isipokuwa CHADEMA ila wameweka swali hilo,kwakuwa TWAWEZA
ni taasis inayothamini midahalo tunawaalika kwenye midahalo ya kutetea
taarifa ya utafiti wao".
Akizungumzia kuhusu UKAWA kupata mwaliko Wa kufanya mdahalo Wa mgombea
wao Wa urais alisema kuwa hakuna taasis yoyote iliyoleta barua kwa
mgombea urais,Edward Lowassa kushiriki kwenye midahalo.
"Utafiti Wa ndani Wa UKAWA uliofanywa na watafiti guru kutoka nje ya
nchi ulionyesha Edward Lowassa atapata kura 74%".alisema Mbatia.
Naye Prof.Baregu alisema kuwa sampuli ya data za utafiti Wa TWAWEZA imechafuliwa kwa makusudi ili kupotosha umma.
"Mtafiti kutoka Oxford University niliongea naye aliona kuwa UKAWA inaweza kushinda ila siyo kwa gap kubwa"alisema Baregu
Mkutano wa UKAWA na waandishi Wa habari kuhusu utafiti wa TWAWEZA

Isikupite taarifa hii kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM)

Chama cha Mapinduzi kinapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa
- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/09/isikupite-taarifa-hii-kutoka-chama-cha.html#sthash.2A5J1iyl.dpufMwenendo wa Kampeni Kwa kifupi, Mgombea Urais, Ndugu John Pombe Magufuli na Mgombea-Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan, wanaendelea vizuri na kampeni. Kila mmoja anafanya mikutano na wananchi kati ya 8 hadi 11 kwa siku na kukutana na maelfu kwa maelfu ya wananchi. Tunawashukuru wananchi wanaokuja kwenye mikutano yetu
. Tunawashukuru pia makada wa CCM wanaojitolea kwa hali na mali kukipigania Chama cha Mapinduzi na kumtafutia kura Ndugu Magufuli. Tunaridhika sana na mwenendo wa kampeni yetu. Katika nusu hii ya pili ya kampeni tutaongeza kasi na msukumo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa mbinu na mikakati mipya. Midahalo ya Wagombea Tumeshangazwa na kauli ya Ndugu Kajubi Mukajanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania kwamba CCM haijathibitisha kushiriki mdahalo. CCM ilipokea mwaliko wa MCT na kuijibu kwa barua ya tarehe 13 Septemba 2015 yenye kumbukumbu CMM/OND/M/190/132 iliyosainiwa na Ndugu Stephen Msami, Msaidizi wa Katibu Mkuu. Barua hiyo ilipelekwa na kupokelewa kwa dispatch ambayo nakala yake tunayo. Baada ya hapo, Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, alifanya kikao na wawakilishi wa MCT katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba ili kutaka kujua zaidi na kutoa maoni ya CCM kuhusu utaratibu mzima wa mdahalo. Katika kikao hicho, ambapo MCT iliwakilishwa na Afisa wake, Ndugu Allan Lawa, pamoja na Ndugu Tido Mhando, CCM ilithibitisha tena kushiriki mdahalo. Tatu, tarehe 16 Septemba 2015, CCM ilitoa kauli rasmi, iliyosainiwa, ikithibitisha kushiriki mdahalo. Kauli ya Ndugu Mukajanga inalenga kuwasaidia kisiasa wale ambao hawajathibitisha au hawana nia ya kuthibitisha kushiriki. Kwa msingi huu, tunaamini ni vyema mdahalo huu ukaandaliwa na ushirika wa taasisi mbalimbali zilizokuwa na nia ya kuandaa midahalo, (kama vile CEO Roundtable, UDASA, Twaweza) ili kuiondolea uwezo taasisi moja, au kikundi cha watu wachache, kuhodhi na kuwa na ukiritimba kwenye jambo hili kubwa na muhimu. CCM inapenda kusisitiza yafuatayo: 1. Ndugu Magufuli amekubali kushiriki mdahalo wa wagombea Urais 2. Mdahalo uwashirikishe wagombea wenyewe na sio wawakilishi wao. 3. Wagombea wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki. Tunapozungumzia mabadiliko katika nchi maana yake ni utayari wa kufanya mambo mapya yenye tija ambayo hayajawahi kufanyika, ikiwemo mdahalo wa wagombea Urais. Wanaohubiri mabadiliko huku wakiogopa kushiriki mdahalo wanahubiri mabadiliko hewa. Utafiti wa TWAWEZA CCM haikushangazwa na matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza yaliyotangazwa jana ambayo yanatoa ushindi wa asilimia 65 kwa Ndugu John Pombe Magufuli dhidi ya asilimia 25 za Mgombea wa UKAWA. Hatukushangazwa na matokeo ya utafiti huu kwasababu tano: 1. Siku UKAWA walipomteua Ndugu Edward Lowassa kuwa mgombea wao ndio siku CCM ilipohakikishiwa ushindi katika uchaguzi wa mwaka huu. CCM hatukumteua kwasababu tuliamini hakuna namna ambapo Watanzania wengi watamchagua. 2. Katika uchaguzi wa mwaka huu CCM tunafanya utafiti wetu wa ndani wa kisanyansi kila wiki kujua mwenendo na mwelekeo wa kampeni na maeneo yanayohitaji nguvu mahsusi. Tangu tuanze utafiti wetu mwishoni mwa mwezi Agosti, karibu kila wiki asilimia za ushindi wa CCM hazijawahi kushuka chini ya asilimia 60 na zimekuwa zinapanda. 3. Kazi kubwa anayofanya mgombea wetu, Ndugu John Pombe Magufuli, na mgombea-mwenza, Ndugu Samia Suluhu Hassan, kuzunguka nchi nzima kwa barabara na kuongea moja kwa moja na wapiga kura inazaa matunda. Wanawafikia wapiga kura wengi, hasa wa vijijini, na wapiga kura hao wanawaelewa. 4. Kampeni kubwa zinazofanywa na wagombea Ubunge na Udiwani wa CCM na makada na viongozi wa Chama katika ngazi zote nchi nzima kila siku kumuombea kura Magufuli nazo zinazaa matunda. 5. Tunaamini pia migogoro ndani ya UKAWA katika kipindi hiki cha uchaguzi iliyopelekea mitafaruku katika kuachiana majimbo na, baadaye, kutokana na uteuzi wa Mgombea Urais wa UKAWA, kupelekea kujiuzulu kwa viongozi wa muda mrefu na maarufu wa UKAWA, Profesa Ibrahim Lipumba na Dr. Wilbrod Slaa, na migongano ndani ya NCCR-Mageuzi, yote haya yamepunguza imani ya wananchi kuhusu uwezo wa vyama hivi kushika dola. Lakini vilevile matokeo ya utafiti huu ni ishara kwamba Watanzania wamempokea na kumuelewa Ndugu Magufuli na wako tayari kumkabidhi nchi. Sisi kama CCM kuna baadhi ya mambo tumeyachukua katika utafiti huu na tutayafanyia kazi ili kujihakikishia ushindi. Tumeshangazwa na taharuki, hasa kutoka miongoni mwa wasomi na wanaharakati, kuhusu matokeo ya utafiti huu. CCM ilitegemea kwamba jamii ya wasomi na wanaharakati ingefurahia utamaduni wa tafiti za kisiasa unaoanza kujitokeza hapa nchini ili siku zijazo tujikite katika kurekebishana kwenye kanuni za utafiti na ithibati na uhakiki wa ubora. Tunasikitika kwamba yanawekwa mazingira ya kutisha na kukatisha tamaa (atmosphere of intimidation) kwa watu wanaotaka kufanya tafiti za kisiasa nchini. Utafiti ni sayansi. Matokeo ya utafiti hupingwa kwa matokeo ya utafiti mwingine, sio kwa kuponda tu au kwa matusi na vitisho. Ni vyema tukajifunza kupokea habari mbaya bila taharuki. Itakumbukwa kwamba, mwezi Agosti 2010, taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Synovate ilitoa utafiti ikionyesha kwamba CCM itashinda Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa asilimia 61. Baadhi ya wana-CCM hawakufurahishwa na matokeo ya utafiiti huo kwasababu waliamini kwamba ushindi wetu ulikuwa ni mkubwa zaidi. Wapinzani waliwalaani, kuwatukana na hata kutaka kuwashtaki Synovate. Kwenye matokeo halisi ya kura, CCM ilipata asilimia zilezile 61 zilizotabiriwa na Synovate. Ni vyema kuweka akiba ya maneno kwenye masuala haya. Imetolewa na: January Makamba Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mjumbe wa Kamati
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko