|
Ni
wakati mwingine tena nikikukaribisha tena wewe msomaji wangu wa makala
hii ya uchambuzi wa miondoko ya muziki wa hapa duniani, karibuni katika
ukurasa huu wa kuelimishana juu ya mambo mbalimbali yanayohusu chimbuko
la mitindo ya muziki wa dansi.
Kwa kawaida tunachagua mtindo mmoja na kuuchambua kwa kina kwa safari
ya vituo visivyopungua kumi, japo wakati mwingine vituo hupitiliza ili
kuweza kutosheleza uchambuzi husika
.
Leo tunaifungua rasmi ile safari ya uchambuzi wa miondoko ya Sebene
Tumeuchambua mtindo huu kwa mfululizo wa jumla ya vituo 13, lakini hadi
sasa ni ‘Gospel’ ndiyo inayoshikilia rekodi kwa urefu wa uchambuzi
ikifuatiwa na taarab, kupitia safu hii leo tutahitimisha tathmini hii
fupi ya kimuhtasari kwa ujumla, wa mambo yote tuliyoyachambua tangu
mwanzo hadi sasa. Tuanze kutiririka katika muhtasari huo tukianzia
tulipoishia wiki iliyopita. Kwani sehemu kubwa muziki huo ukiwa
umeshajipatia umbo lake kwa vionjo zaidi ya vitano kwani kizazi kipya
cha kikongo kikachanganya miondoko miwili, ya taratibu na haraka na huo
ndio wakati wapiga solo walitukuzwa sana na kutajwatajwa mno kwenye
nyimbo. Baadaye walivuta kasi kabisa na kuamua kuunda bendi zao
binafsi, tuliwataja watu kama Diblo Dibala, hapa nyumbani unakumbuka
mambo ya kutajwa sana kina Vumbi Dekula Kahanga? Tukaja kuona
kuondolewa kwa ufalme huo wa wapiga solo na baadaye kuja ufalme wa
marepa kuziba nafasi zao na kuanza kuwapo kwa wanenguaji wa kulipwa
(professional). Vikaja vionjo vya mwisho mwisho vya kiufundi zaidi
wakati Wakongomani walipojifunza kurekodi vizuri zaidi na kuchanganya
sauti vyema zaidi jukwaani kutokana na kuona ufundi wa wanamuziki
waliotembelea kwao. Manu Dibango kutoka Cameroon, Jimmy Cliff
kutoka Jamaica na Vyonne ‘Machaka’ Chakachaka kutoka Afrika ya Kusini ni
wa kupigiwa mfano. Tuliona pia kukubalika kwa muziki wa mitindo mingine
huko kwao, si masebene tu kama wengi wetu tunavyofikiria, hapo tulitoa
mfano wa simanzi zilizowagubika kutokana na kifo cha Lucky Dube.
Tukaja kuona mgawanyiko maridhawa wa mpangilio wa nyimbo na gitaa
lilirudi kwa kasi kubwa, lakini baada ya kipande chake cha kuchezesha,
lilizama kwa chini katika sebene na kupisha marepa wakiongozwa na wapiga
‘drums’ kuwaongoza wanenguaji. Tukakumbushana mambo ya akina Yondo
Kusala. Ubunifu na makali ya wapiga solo ndio uliouza miondoko
hiyo, sanjari na mitindo ya nguo ya mabuga na raizoni, mambo ya ‘Fuka
Fuka’ enzi hizo. Hapa ndipo sebene la kisasa hasa lilipozaliwa,
ngoma ya ‘snare’ ikachukua nafasi ya ‘kavasha’ kwa mapigo ya kubamiza
na mapigo ya solo ya kudonoa yaliyokuwa ya kasi yalijitofautisha na
mapigo mazito ya taratibu ya magitaa manne basi hapo tungo zikawa na
maneno machache na chemka ikawa ndefu, Sebene likawa moto kabisa.
Na ndipo biashara ikaingia katika muziki huu na kushamiri zaidi kuliko
ilipoingia pale awali, na ndipo Usambazaji wa muziki huu ukasababisha
‘mapromota’ kuukimbilia hasa kutokana na kupendwa na mashabiki kutokana
na mabadiliko ya mapigo yaliyofanywa na wanamuziki wa kizazi kipya cha
Kikongo.
Sebene, muziki kutokea jukwaani ukaenda studio na kutoka huko
ukawafikia walaji ‘wanunuzi’ wa muziki huo, Upepo mkubwa wa mabadiliko
ukawalazimisha hata wanamuziki wakongwe kujikongoja na mifumo mipya,
maana wanamuziki waliokuwa ugenini walipata ‘promosheni’ kubwa na
kuvumisha upepo wa mabadiliko hadi huku nyumbani. Kizazi kipya
cha Wakongomani kikasababisha kuundwa kwa bendi za Kikongo, hatimaye
bendi mchanganyiko za wazalendo na Wakongo na kuwateka mashabiki kwa
mambo mapya, na tukaona mambo ya ‘Ikibinda Nkoi’ ya Diamond Sound na
bendi nyingine kama Beta Musica na FM Music Band. Kuingia kwa
nguvu kwa miondoko mikali ya kizazi kipya cha kikongo kukarudisha hadhi
ya wakongomani iliyoanza kupotea hapa nchini. Kukatika kukawa kwa jinsia
zote kwa mujibu wa mambo hayo mapya, yaani wake kwa waume wote
walikatika. Uhuru wa kibiashara wa kuingiza bidhaa mbalimbali
zikiwamo zana bora za muziki, ulisababisha kuwa na vikundi vyenye
midundo bora na zana za kisasa kabisa. Lakini bado kulikuwa na
‘rapu’ tenge hata nyimbo bado ziliimbwa kwa ‘kibudu’ Kiswahili kibovu
cha Kikongo, Ukongomani ulihusudiwa mno na watu wakajiita ‘mapapaa’
lakini hatimaye taratibu mchanganyiko huo ulianza kupotea, hasa kutokana
na kuwa na makundi yaliyoundwa na wanamuziki mchanganyiko wa kikongo na
kizalendo. Bendi zilizokuwapo tangu zamani kabla ya kuingia
mambo hayo mapya zilibadilika kwa kujibadilisha majina na kupiga
mirindimo ya Kiswahili iliyo kwenye mirindimo ya Kikongo.
Tukakumbushana ngoma za maghorofani, mambo ya ‘Ngulupa Tupa Tupa’ na
‘Tukunyema mpaka chini’. Tukawakumbuka wanenguaji wa kwanza kabisa wa
mitaani akina Kibengo Shabani al-maarufu kama ‘Super Cadet’. Tija katika
muziki huo ilileta ubunifu uliowakaba Wakongomani kutoka kwa wanamuziki
wazalendo. Upinzani huo wakati fulani nusura uvuke mstari wa mashindano
ya kisanaa na kutaka kugeuka uhasama. Uchambuzi wetu
ukakanusha kauli za wanamuziki wa kigeni wa Kikongo wenye makao yao
Ulaya, ambao kila walipokuja walidai hawaujui muziki wetu na hawajawahi
kuusikia. Tukagundua kuwa hata bendi za Wakongomani zilizoko nchini hivi
sasa, zinategemea sana lugha ya Kiswahili kuukubalisha muziki wao.
Kama ambavyo wao walidai kuwa wanamuziki wetu wanapiga miondoko ya kwao
ila wanaimba kikwetu na tukaona ubunifu mpya ulioweka uwiano wa
mirindimo iliyoleta kitu kipya kabisa na tofauti ambacho kiko kati kwa
kati. Ni masebene, lakini si ya Kikongo wala kitanzania sana
japo yanaweza kuelemea upande wowote kati ya hizo mbili kutokana na
muundo wa bendi. Hiyo ni kwa kuwa hakuna kujitegemea kabisa katika
muziki, kwamba karibu mitindo yote ya muziki duniani inatokana na kukopa
vionjo mbalimbali. Kwa ufupi, hayo ndiyo yote tuliyoyaona japo
hatukumaliza kila kitu, maana historia ya muziki wenye silika za
Kikongo ni ya kina sana. Washkaji zetu wa Darhotwire
aliotuhabarisha na hii wanamaliza kwa kusema, Wao wamezoea mitindo mingi
mno, hiki tunachokiona ni sehemu tu ya mambo yao, tena ni kile
kilichochanganyika na vionjo vya kimataifa. Ila tukirudi kwenye
utamaduni wao, jenga picha wewe mwenyewe msomaji, maana wao wana
makabila takriban kama 400 hivi. |
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Blogger Comment
Facebook Comment