MSAMBICHAKA MWENYE NGUO NYEUSI AKIWASALIMIA WANANCHI WA LUDEWA |
Na Barnabas njenjema ,Ludewa
Mara baada ya mgombea wa ubunge jimbo la ludewa kupitia chadema Bathromeo msambichaka kushinda pingamizi aliyowekewa na mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi Deo Filikunjombe mgombea huyo amezindua kampeni za uchaguzi huku akiwahakikishia wananchi kushinda kwa kushindo
Chama cha demokrasia na maendeleo chadema wilaya ya ludewa katika mkoa wa njombe hapo jana september 03 mwaka huu kimezindua rasmi kampeni zake za mgombea ubunge katika maeneo ya viwanja vya sokoni Ludewa mjini uzinduzi ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho kutoka ludewa na uongozi ngazi ya mkoa.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo baadhi ya viongozi wa chadema pamoja na wagombea kiti cha udiwani kupitia chama hicho katika kata mbalimbali wilayani ludewa walisema kua mwaka huu 2015 ni mwaka wa wananchi kuamua na kufanya mabadilio ili kuweza kupata viongozi bora wa kuweza kutatua kero na changamoto zao wanazo kabiliwa nazo ndani ya Ludewa.
Viongozi hao waliongeza kuwa kunabaadhi ya wagombea kiti cha udiwani wa kata mbalimbali wilayani ludewa wamewekewa pingamizi zisizo kuwa na maana hivyo wao wanajua hizo ni mbinu potofu za vyama vingine kutaka kuingia madarakani kwa nguvu bila kujali maslahi ya wananchi.
Kwa upande wake mgombea kiti cha ubunge kupitia chama hicho cha chadema ambae anawakilisha umoja wa katiba ya wananchi ukawa wilaya ya LUDEWA bw, Bathromew msambichaka Mkinga alisema kuwa aliwekewa pingamizi na mgombea wa ccm wilaya ya ludewa mh, Deo Filikunjombe hivyo aliamua kukata rufaa na rufaa hiyo imekubaliwa na tume ya taifa ya uchaguzi hivyo ameruhusiwa kuendelea na kampeni zake huku akimtaka msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Ludewa kuwa makini hasa kwa kutenda haki kwa vyama vyote vya siasa hasa kwa kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu wa october 25 mwaka huu.
Aidha mgombea huyo aliongeza kuwa mara baada ya kukamilisha taratibu zote na kurejesha fomu ya serikali kwa msimamizi badae msimamizi wa uchaguzi alimwambia kuwa amewekewa pingamizi na mgombea wa ccm Deo Filikunjombe kuwa kunabaadhi ya fomu namba kumi haikuonekana kitendo ambacho mgombea huyo amekanusha na kusema kuwa msimamizi huyo wa uchaguzi aliificha fomu yake ili kumtangaza mgombea wa ccm kuwa amepita bila kupingwa.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ludewa bw, Willium Waziri ambae pia ni msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la uchaguzi ludewa alimtangaza Nd, Deo Haule Filikunjombe kuwa amepita bila kupingwa na kumukabidhi barua aliyomuandikia kuwa ametangazwa kupita bila kupingwa hatua ambayo ilipingwa vikali na vyama vya upinzani Wilayani Ludewa.
0 comments:
Post a Comment