AZAM FC wapeleka malalamiko ya udhaliilishwaji wa mchezaji wao


Klabu ya AZAM FC imepeleka malalamiko yake ya kwenye kamati ya saa 72 ya bodi ya ligi juu ya kitendo cha udhalilishaji kinachosadikiwa kufanywa na mchezaji wa MBEYA CITY kwa mchezaji wao JOHN BOCCO
AZAM FC wapeleka malalamiko ya udhaliilishwaji wa mchezaji wao
Klabu ya AZAM FC imepeleka malalamiko yake ya kwenye kamati ya saa 72 ya bodi ya ligi juu ya kitendo cha udhalilishaji kinachosadikiwa kufanywa na mchezaji wa MBEYA CITY kwa mchezaji wao JOHN BOCCO
Akizungumza na TBC afisa habari wa klabu hiyo JAFFARI IDDI MAGANGA amesema wamechukua uamuzi wa kumwandikia mwenyekiti wa kamati hiyo ya bodi ya ligi malalamiko yao huku wakisubiri maamuzi ya kamati ya nidhamu ya TFF.
Siku ya jumapili kwenye uwanja wa AZAM COMPLEX katika mchezo wa ligi kuu kati ya AZAM na MBEYA CITY mchezaji JUMA NYOSO wa MBEYA CITY inasadikiwa alimfanyia kitendo cha udhalilishaji mchezaji JOHN BOCCO wa AZAM kwa kumgusa sehemu za makalio na kidole cha kati.
Kanuni ya ligi inasema mchezaji atakayepatikana na hatia ya kufanya makosa makubwa ya kimaadili au kinidhamu au kibaguzi au ya kidhalilishaji au hata yatakayotafsiriwa kuwa niukiukaji mkubwa wa taratibu za mchezona ubinadamu atatozwa faini kati ya shilingi MILIONI MOJA mpaka milioni TATU au na kusimamishwa kushiriki michezo 3mpaka 10 ya klabu yake au kufungiwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja na miwili.
Wakati huo huo klabu hiyo imesema ina majeruhi wawili tu KIPRE BALUU na MCHA VIALI kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya COASTAL UNION utakaochezwa kwenye uwanja wa mejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo wa kesho



Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment