MBUNGE
wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amewashukuru wana Chama wa chama
cha mapinduzi (CCM) kwa kura nyingi za ushindi walizompa na kuwa ahsante
yake Kwao ni kuwatumikia kwa kasi zaidi
Filikunjombe alisema hadi ushindi huo umempa faraja zaidi ya kuona wazi wazi mapenzi ya wananchi wake dhidi Yake
Mbunge huyo aliyasema hayo jana baada ya kupokea matokeo ya ubunge katika kata 23 Kati ya 26 za jimbo hilo la Ludewa
Kuwa ushindi ambao ameupata wa kura zaidi ya 18,300 ni ushindi mkubwa ukilinganisha na ule wa kura 770 aliopata mtu wa pili na kura 250 alizopata mtu wa tatu
" Nimefurahishwa sana na kura nyingi nilizopata kweli nimeamini wananchi wangu wapo pamoja na wametambua Kazi ya maendeleo niliyowafanyia"
Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Ludewa Bw Enzi Eliasi alisema kutokana na Joghorafia ya Wilaya ya Ludewa ni matokeo ya kata 23 Kati ya 26 ndio yamepatikana na Kati ya kata hizo zote Filikunjombe anaongoza kwa kura 18,290 wakati injinia Zephania Mpangala akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 770 na kepten ( mstaafu) Jacob Mpangala akipata kura 250
Alisema matokeo ambayo bado ni kata ya Lifuma,Kilondo na Makonde
0 comments:
Post a Comment