CUF kukutana kwa dharura kumjadili Prof.Lipumba

Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba alipotangaza kujiuzulu jana.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba alipotangaza kujiuzulu jana.
Kufuatia mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Lipumba kutangaza kujiuzulu jana  Katibu Mkuu Maalim Seif Shariff Hamad  ameagiza kuitishwa kwa vikao vya dharura vya Kamati ya Utendaji ya Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa siku ya Jumapili, tarehe 9 Agosti, 2015.

Aidha kikao hicho  kitajadili hatua hiyo na kufanya maamuzi juu ya hatua muafaka zinazopaswa kuchukuliwa katika kipindi hiki hadi hapo Chama kitakapomchagua mwanachama mwengine kujaza nafasi hiyo ya Mwenyekiti.
Kwa mujibu wa taarifa iiyotolewa na  ismail jussa ambaye ni kaimu mkurugenzi wa habari, uenezi na mawasiliano na umma amesema kwamba Katika kipindi hiki, Chama kinawataka wanachama na wapenzi wake wote kuwa watulivu na wavumilivu na kusubiri maelekezo ya vikao vya juu vya kitaifa vya Chama.
Akizungumzia kujiuzulu kwa Prof.Lipumba Jusa amesema Chama hicho  kimezipokea taarifa hizo na kinayaheshimu maamuzi yake  pia ni   haki yake ya kikatiba na haki ya kidemokrasia kufanya maamuzi anayoyaona yana maslahi kwake.
Katika hatua nyingine amewahakikishia wanachama kuwa  CUF itaendelea na shughuli zake kama Chama na pia kama mshirika katika UKAWA ambayo CUF ilikuwa ni katika waasisi wake.
“Tunawahakikishia wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla kwamba CUF itatumia nguvu, uwezo, juhudi na maarifa yake yote kuhakikisha kwamba inaulinda UKAWA ambao unaonekana kuwa mwiba kwa CCM.”Amesema Jussa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: