TAARIFA RASMI YA UKAWA KUHUSU MGOMBEA URAIS WAO WA OCTOBA MWAKA HUU, NA MAJIBU YA KAULI YA GOLI LA MKONO YA NAPE NNAUYE


Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) na vyama washirika vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA ) wamesema kuwa wako imara na wamejiandaa vyema kushinda katika uchaguzi mkuu ujao kwa kukiondoa madarakani chama cha mapinduzi, licha ya kauli inayodaiwa kutolewa na katibu mwenezi wa chama hicho Nape Nnauye wakati wa ziara ya katibu mkuu wa chama hicho mkoani Mwanza kwamba CCM itashinda hata kwa goli la mkono.

Kauli hiyo imetolewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya magomeni kirumba jijiji Mwanza na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa ambapo katika mkutano huo mwenyekiti wa taifa wa Chadema Mh.Freeman Mbowe amewatambulisha rasmi waliokuwa wabunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Mh. James Lembeli na Mh. Esther Bulaya ambao wamehamia Chadema, huku akiwatahadharisha wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge kutokubali kununuliwa kwa lengo la kukihujumu chama hicho. 

Awali mwenyekiti wa taifa wa baraza la wanawake wa Chadema (BAWACHA) Halima Mdee, naibu katibu mkuu wa chama hicho upande wa Zanzibar Salum Mwalim pamoja na mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu wamesema wakati umefika kwa watanzania kuchagua viongozi wanaokubalika na wenye uchungu na raslimali za taifa kwa uhuru bila kutishwa kwani saa ya ukombozi kupitia sanduku la kura utajulikana oktoba 25 mwaka huu.

Kwa upande wao waliokuwa wabunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi James Lembeli wa jimbo la Kahama na Esther Bulaya viti maalum umoja wa vijana CCM mkoa wa Mara nao wametumia mkutano huo kueleza kilichowasukuma kujiunga na Chadema
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: