Na. Lakia Ndwellah wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Mnamo tarehe 28.7.2015
majira ya jioni JOSEPH ELIAZA CHILONGANI alifika katika kituo cha Polisi
Kibaigwa akilalalmika kuwa wakati wakiwa kwenye kampeni za kujinadi kwa
wanachama kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea ubunge kupitia CCM
alishambuliwa kwa fimbo sehemu za kichwani na tumboni na JOB YUSTOO
NDUGAI (MB).
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamiz wa Polisi DAVID
MISIME – SACP amesema mtu huyo aliyejeruhiwa alipewa PF3 na kupelekwa
katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa uchaguzi wa madaktari na
matibabu. Amelazwa na anaendelea na matibabu hadi sasa, hali yake
anaendelea vizuri.
Kamanda
MISIME amesema uchunguzi wa malalamiko hayo unafanyiwa kazi kwa kupata
maelezo ya watu walio kuwa kwenye mkutano huo wa kampeni na
ukikamilishwa jalada litapelekwa kwa Wakili wa Serikali kwa hatua zaidi
za kisheria.