Jeshi la Kenya latumia Bilioni 1.1 kununua magari ya kivita yasiyo na viwango.

A German Henschel Wehrtechnik Transportpanzer 1 (Fuchs) armored personnel carriers, part of the coalition forces, parked at Bagram Air Base (AB), Afghanistan, during Operation ENDURING FREEDOM. (SUBSTANDARD)
Moja wapo ya magari ya kivita aina ya Armoured Personnel Carriers (APCs).
Mkaguzi Mkuu nchini Kenya Edward Ouko amehoji matumizi ya shilingi bilioni 1.1 za Kenya yaliyofanywa na Jeshi la Ulinzi la Kenya kununua magari 32 ya kivita yenye silaha (ACP’s).
Bw. Ouko amesema ripoti ya mwisho ya ukaguzi haijatolewa kwa ajili ya ukaguzi, japokuwa kiasi chote cha fedha za makubaliano kimeshalipwa.

Bila kupatikana kwa ripoti hiyo, Bw. Ouko amesema sio rahisi kuthibitisha iwapo mkataba ulitekelezwa kwa maridhiao ya Wizara ya Ulinzi na hivyo walipa kodi kufaidika na fedha zao.
Manunuzi hayo yamefanyika kupitia zabuni iliyozuiliwa, lakini Wizara imeeleza kuwa kampuni iliyohusika ilishinda zabuni hiyo kwa ushindani.
Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa magari hayo 32 ya kivita yaliyoletwa mwaka 2008, yalipelekwa nchini Sudan Kusini sanjari na mkakati wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini na bado yapo nchini humo.
Zaidi ya hapo taarifa hizo zinasema, Umoja wa Mataifa umegundua kuwa paa za  magari hayo ya kivita zinavuja hivyo maji huingia ndani, pia yana matairi yasiyoweza kudhibiti pancha kwa kujiziba yenyewe.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: