Akizungumza na Wananchi leo Mkoani Mwanza mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe amesema kwamba kupanda kwa gharama za maisha kumetokana na serkali iliyopo madarakani huku akitolea mfano kuwa mwaka 2010 wananchi waliweza kununua kilo ya Nyama kutokana na maisha yalikuwa chini ila hivisasa bei ya vitu iko juu.
Naye Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk .Wildroad Slaa amesema kwamba Chama cha Mapinduzi kimewapokonya wananchi serikali yao na kuifanya kuwa ni ya watu wachache na kuwataka kuichagua Chadema ili iweze kuwarudishia wananchi serikali yao ilipokwa kwa muda mrefu.
Katika mkutano huo Chadema imewatabulisha wanachama Wapya ambao ni Ester Bulaya pamoja na James Lembeli.
Chama hicho pia kimewataka wananchi kuwa wapole kwani kinatarajia kumtangaza mgombea wake wa urais mwezi agosti tarehe 4 huku kikisisitiza kuwa hakifanyi mambo eti kwa vile chama fulani kimefanya.
Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa Mbunge wa Monduli Edward Lowassa naye ni mmoja wa wanasiasa wanaotaka kuhamia katika chama cha Chadema kufuatia jina lake kukatwa katika kinyang’anyiro cha urais kilichofanyika wiki moja iliyopita ambapo Dk.John Pombe Magufuri ameibuka kidedea. Lakini hata hivyo hajaweza kuthibitisha madai hayo.
0 comments:
Post a Comment