Chama cha ACT-Wazalendo kintarajia kutoa fursa kwa watangaza nia wa nafasi mbalimbali katika mkutano wake wa kitaifa utakaofanyika tarehe 13 mwezi huu. Hatua hiyo inafuatia joto la urais kuanza kupanda ndani ya vyama mbalimbali vya kisiasa nchini kikiwemo chama tawala cha Mapinduzi (CCM).Kwa mujibu wa Katibu Mawasiliano na Uenezi wa Chama wa ACT –wazalendo Sabini Richard amesema chama hicho kimejipanga kushiriki katika uchaguzi mkuu hivyo kutakuwa na mkutano mkuu utakaofanyika mkoani Tabora.Katika mkutano huo watahuisha azimio la Arusha lengo likiwa ni kudumisha misingi ya amani, udugu na uzalendo kwa lengo la kuwaunganisha watanzania pamoja na kuenzi harakati za ukombozi barani Afrika.Katika hatua nyingine, Richard amesema katika mkutano huo hicho wanatarajia kusimamishawagombea katika nafasi ya Urais na Wabunge na madiwanikatika majimbo yote nchini.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment