Ukawa kufichua siriya mgombea wao mwezi huu

Umoja wa Katiba ya wananchi Ukawa umesema kwamba mgombea urais kupitia umoja huo atapatikna wakati wowte kuanzia sasa.Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia akihojiwa katika moja ya kipindi cha televisehini hivi karibuni amesema mchakato wa kumpata rais ndani ya umoja huo unakwenda vizuri na hilo linatokana na UKAWA kuaminiana.Amesema kuwa wapo watu wengi ndani ya UKAWA wanaoweza kugombea nafasi ya urais na si lazima rais awe mwenyekiti wa chama chochote. “Naomba tofauti zisiwepo ndani ya UKAWA ili tuweze kumpata mgombea mmoja wa nafasi ya urais ambaye atakuwa mwadilifu na mzalendo kwa taifa lake.Kwa uande wake amesema yeye binafsi yupo tayari kutogombea nafasi yoyote hata ya udiwani iwapo hatapewa nafasi ya kuratibu shughuli za uchaguzi ndani ya umoja huo ilikuhakikisha mambo yanakwenda vizuri.Hadi sasa kwa asilimia 90 UKAWA imekamilisha taratibu za kuwapata wagombea katika baadhi ya majimbo na kata kwa ngazi za ubunge na udiwani, hivyo aliwataka Watanzania kuwaunga mkono kwa jitihada zao.“Kwa hali halisi inaonyesha kwamba Watanzania wengi wanapenda UKAWA kuliko chama kimoja, hivyo ni lazima viongozi wa umoja huo kutambua kwamba wasiingize tofauti zao.”Amesma MbatiaAmesisitiza kuwa UKAWA si mali ya chama, bali ni mali ya Watanzania wote na kuwataka wanachama wa CCM wenye nianjema kujiunga na umoja huo sasa na kutosubiri hadi washindwe ndani ya CCM.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: