Stars yaendelea kujifua kuwakabili Misri

Juzi kikosi cha Stars kilifanya mazoezi majira ya saa 9 mchana katika uwanja wa Taifa wa Ethiopia (Addis Ababa) ambao pia unatumiwa na timu yao ya Taifa kwa mazoezi.Taifa Stars ambayo imeweka kambi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia inajiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017 dhidi ya timu ya taifa ya Misri.Daktari wa Taifa Stars, Billy Haonga amesema hali ya hewa ya Addis Ababa ni nzuri kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri, kutokana na timu kufanyamazoezi katika ukanda wa juu (mwinuko kutoka usawa wa bahari) hali itakayopelekea wachezaji kuwa fit kwa ajili ya mchezo.Hali ya hewa ya Alexandria ni yakawaida, hakuna baridi sana kutokana na kuzungukwa na bahari ya la Mediterania, hivyo kipindi cha wiki moja tutakachokuwa kambini hapa Addis Ababa tunatarajiwa vijana watakua vizuri kabisa kw aajili ya mchezo” Alisema Haonga”.Wachezaji wote wa Taifa Stars waliopo kambini Addis Ababa wapo katika hali nzuri, kiafya, kifikra na morali ya juu kujiandaa na mchezo dhidi ya Mapaharao.Wenyeji Chama cha Soka cha Ethiopia (EFF) wanaangalia uwezekano wa Taifa Stars kupata mchezo mmoja wa kirafiki wa kujipima nguvu kablaya kuelekea nchini Misri.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: