MWENYEKITI BAVICHA KIJIJI CHA LUANA AWATAKA LUDEWA KUTOMPOTEZA FILIKUNJOMBE

Na MatukiodaimaBLOGMWENYEKITI wabaraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA)kijiji cha Luana wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Bw Kalolo Nkwera amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) kwa jitihada zake za uboreshaji wabarabara za wilaya ya Ludewa ikiwemo barabara ya kijiji hichoyenye urefu wa kilomita 2aliyoichonga mbunge huyo kwa kushirikiana na wanakijiji kwa gharama ya zaidi ya Tsh milioni 54.Bw Nkwera alisema kuwa jitihada zilizofanywa na mbunge Filikunjombe katika wilaya ya Ludewa ni kubwa na kila mwananchi wa Ludewa na wasio wa Ludewa ambao wanafika wilayani humo ni mashahidi wa maendeleo ya sasa ya wilaya hiyo na wao kama wapinzani wanatambua mchango mkubwa wa mbunge huyo katika maendeleo hivyo hawana sababu ya kutafuta mbunge zaidi nje ya Filikunjombe.Mwenyekiti huyo wa BAVICHA alisema toa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wanahabari baada ya kushirikiana na mbunge huyo na wananchi wengine katika shughuli ya kimaendeleo ya kuchimba mifereji ya kupitisha maji kweye barabara hiyo mpya ." mimi hapa na baadhi ya wananchi hapo ambao wamekuja kushirikiana na mbunge Filikunjombe katika uchimbaji wa mifereji ya kupitisha maji katika barabara hii ni watu wa upinzani kama mimi ni mwenyekiti wa BAVICHA katika kijiji hiki ila katika masuala ya kimaendeleo mambo ya itikadi za vyama tunaweka kando na kufanya maendeleo .......hii barabara tunapita wote hivyo hatuwezi kuwa wapinzani wa maendeleo yetu"Bw Nkwera alisema kwa kazi iliyofanywa na mbunge huyo katika jimbo la Ludewa kwa kipindi cha miaka 5 ni kubwa zaidi na inaweza imezidi hata ile ya wabunge waliokaa madarakani zaidi ya miaka 40 bila kufanya kazi kubwa kama hiyo ya mbunge wa Ludewa.Hata hivyo alisema ili Ludewaizidi kusonga mbele zaidi hakuna sababu ya wana Ludewa kufanya siasa za maeneo mengine za kuvutana kwenye mambo ya maendeleo kwani kufanya hivyo ni kujikwamisha zaidi katika maendeleo kama ilivyo kwenyemajimbo mengine ambayo wabunge wanafanya kazi katika mazingira magumu na wafuasi wa chama cha upinzani hawatakiwi katika shughuli za CCM na wale wa CCM hivyo hivyo japo kwa Ludewa kwenye mambo ya kimaendeleo ni wananchi wotena vyama vinawekwa kando.Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Luana Bw David Luoga alisema kuwa wananchi hao kamwe hawatamsahau mbunge huyo kwani ameweza kuwaharakishia maendeleo ya kijiji hicho kwa kufikisha umeme na kuwatengenezea barabara hiyo ya Malatu - Itungi ambayo ilikuwa haipitiki japo inaelekea katika taasisi mbali mbali kama nyumba za ibada, soko, Zahanati na shule ila serikali ya wilaya haikuona sababu ya kuitengeneza hadi wananchi hao walivyoomba kwa mbunge huyo katika mkutano wao wa hadhara uliofanyika miezi mitatu iliyopita .Bw Luoga alisema toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961kijiji hicho hawajapata barabara nzuri kama hiyo ambayo ni barabara muhimu ambayo haikupewa umuhimu wowote na serikali ya wilaya yaLudewa.Hivyo alisea ahsante yao kwa mbunge wao kwa kuwaletea maendeleo ni kuona wanamchagua kwa kura nyingi zaidi ili kuendelea kuwa mbunge kwa vipindi vingine 15 ama zaidi na kuwa kipimo chake kilikuwa ni miaka mitano hii ambayo ameonyeha ufaulu wa zaidi ya asilimia 100hivyo kama kijiji wananchi wameweza kuchangishana na kupata kiasi cha Tsh 100,000 kwa ajili ya kwenda kuchukuliafomu muda wa kufanya hivyo utakapofika.Kwa upande wake mbunge Filkunjombe pamoja na kuwapongeza wananchi hao wakiwemo wale wa Chadema ambao walijitolea kushirikiana nae katika ujenzi wa barabara hiyo bado alimpongeza mkurugenzi wa kampuni ya barabara ya Boimanda chini yamkurugenzi wake Nicholaus Mgaya kwa kuendelea kuwa mzalendo na wilaya ya Ludewa kwa kujitolea mitambo ya kuchonga barabara hiyo bila malipo.Alisema ni wakandarasi wachache sana wazalendo ambao wanajitolea kwa wananchi kama hivyo na kuwa kampuni hiyo si tu imekuwa ikijitolea katika jamii bali ni moja kati ya kampuni za kizalendo ambazo zinafanya kazi ya ujenzi wa barabara kwauaminifu mkubwa bila kulipua kama zilizokampuni nyingine zaukandarasi ambazo hugeuza wilaya hiyo ya Ludewa ni shamba la bibi kwa kujenga barabara kwa kiwango cha chini ili mradi wachume pesa.Mbunge Filikunjombe aliwatakawananchi hao wa Luana kutunza barabara hiyo badala ya kuiharibu kwa kupitisha mifugo na kuwa kutengenezwakwa barabara hiyo kutapunguza maswali ya wananchi katika mikutano ya hadhara kwa wananchi hao kila mkutano kutoa kilio cha barabara hiyo huku akisisitishakuwa kero zipo nyingi haziwezi kumalizika zote kwa wakati mmoja japo kwa kuchagua moja moja ipo siku zitamalizika zote ."Leo kikao cha bunge kinaendelea bungeni ila nimeona ni vizuri kukimbia mara moja kuja kutatua kero hiyo ya barabara ambayo ilikuwa ikiwatesa wananchi wangu kwanza .....kwani ubunge huu ni wa wananchi hivyo lazima pale ninapoweza kuwasaidia kero zao"Wakati huo huo mbunge Filikunjombe amewapongeza wananchi wa Luana kwa kumchangia kiasi hicho cha pesa za kuchukulia fomu pia kumpongeza mwenyekiti wa BAVICHA kwa kujitoa kwake katika shughuli za maendeleo pasipo kutanguliza itikadi za chama chake na kuwataka wana Ludewa kushikamana katika mambo ya kimaendeleo badala ya kujikita katika siasa za kupinga maendeleo kama ilivyobaadhi ya majimbo hapa nchini.MWISHO
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: