Wakati Nasibu Abdul ‘Diamond’ akijinadi kwa mbwembwe kuwa anategemea
kiumbe kutoka kwa mwandani wake Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’,
ubuyu mpya wa mjini unadai kuwa mimba aliyobeba mrembo huyo si ya
Diamond, Amani limemeza sababu za kutosha. 
Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’.TUJIUNGE NA CHANZOKwa mujibu wa chanzo chetu kilicho karibu na Diamond anayesumbua kwa sasa na wimbo wake wa Nana, tangu habari ya ujauzito wa mlimbwende huyo mwenye asili ya Uganda ianze kupamba vyombo mbalimbali vya habari, watu walio karibu na staa huyo hawakuziamini.“Hatukuamini sababu kwanza muda ambao Diamond alikutana na Zari ulikuwa mchache ukilinganisha na miezi mitatu ambayo mimba ilibainika. Watu wa karibu tulikuwa tunajua lakini tulikuwa tunashindwa pa kuanzia kusema.MITANDAO YAWASAIDIA“Sijui bwana nani alivujisha hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii ndiyo maana hata sisi sasa tukawa radhi kufunguka. Tena imeeleza mambo ya ukweli tupu ambayo sisi tulikuwa tunayajua,” kilisema chanzo chetu.IMESEMAJE MITANDAO?Watumiaji mbalimbali wa mitandao ya kijamii wametoa maoni kuwa, kwa asilimia 90 mimba ya Zari si ya Diamond na kuna uwezekano ana tatizo la uzazi kwani hata mpenzi wake wa zamani, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ aliwahi kukaririwa akisema Diamond hajampa ujauzito kama yeye alivyokuwa akijisifia kuwa amempa halafu ukatoka.
Diamond
akibusu tumbo la Zari.ANA TATIZO?“Yawezekana ana matatizo. Haiwezekani
aseme amempa mimba Jokate akaitoa halafu mwenyewe akatae. Kama
mnakumbuka hata alipomwagana na Penny (Penniel Mungilwa), alisema ametoa
mimba yake kitu ambacho mrembo huyo alikikanusha na kumtaka kama kweli
ana ushahidi wa hospitali aliyoitumia kutoa mimba ampe,” alieleza mdau
mtandaoni.MWINGINE AKUMBUSHIA YA MUME WA ZARIKama hiyo haitoshi,
mchangiaji mwingine katika mitandao hiyo ya kijamii alishibisha hoja ya
mimba ya Zari si ya Diamond kwa kukumbushia suala la aliyekuwa mume wa
Zari, Ivan Semwaga kufunguka kuwa kamwe Zari hawezi kumzalia
Diamond.“Mume wa Zari alikuwa anaujua ukweli wa mimba ya Zari (huenda ni
yake) ndiyo maana alinukuliwa katika vyombo mbalimbali vya habari
pasipokuwa na shaka yoyote, kama hamuamini, akijifungua kipimo cha DNA
kitamaliza ubishi,” alichangia mtu huyo.
Zari
akiwa na Katunzi.KATUNZI ATAJWAUshahidi wa mimba hiyo kuwa si ya
Diamond ulizidi kumwagwa mtandaoni kuwa Diamond hakuwa mtu wa kwanza
kuonana Zari kwani alitanguliwa na mfanyabishara maarufu Bongo, Mzamili
Katunzi ambaye inasemekana ndiye aliyemfata Bongo kisha baadaye
akakutana na Diamond.“Mtu akiniambia hiyo mimba ni ya Katunzi naweza
nikakubali sababu ndiyo mtu wa kwanza kukutana na Zari lakini Diamond
hana chake pale, si unakumbuka Global (Kampuni ya Global Publishers)
waliwahi kutoa picha ya zamani ya Katunzi akiwa na Zari? Tujiongeze,”
alichangia mchangiaji mwingine mtandaoni.KATUNZI ANASEMAJE?Mwanahabari
wetu alimtafuta Katunzi kujua anazungumziaje kutajwa kwenye ujauzito huo
ambapo alijibu kwa kifupi:“Nani kawaambia? Hivi si mnajua mimi nina
familia yangu? Kwa nini msimuulize mama kijacho mwenyewe (Zari). Mama
mtoto ndiye anayejua ukweli wote.”
DIAMOND
SASAKwa upande wake Diamond alipotafutwa na mwanahabari wetu juu ya
habari hiyo, alisema maneno kwamba mimba si yake si mageni lakini
hayatilii maanani sababu hayana ukweli wowote.“Watu tu wenye roho mbaya
ndiyo wanaongea maneno hayo, ninavyojua mimi tumbo lile linanihusu kwa
asilimia mia moja,” alisema Diamond
Article Source: BongoSwaggz
Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’.TUJIUNGE NA CHANZOKwa mujibu wa chanzo chetu kilicho karibu na Diamond anayesumbua kwa sasa na wimbo wake wa Nana, tangu habari ya ujauzito wa mlimbwende huyo mwenye asili ya Uganda ianze kupamba vyombo mbalimbali vya habari, watu walio karibu na staa huyo hawakuziamini.“Hatukuamini sababu kwanza muda ambao Diamond alikutana na Zari ulikuwa mchache ukilinganisha na miezi mitatu ambayo mimba ilibainika. Watu wa karibu tulikuwa tunajua lakini tulikuwa tunashindwa pa kuanzia kusema.MITANDAO YAWASAIDIA“Sijui bwana nani alivujisha hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii ndiyo maana hata sisi sasa tukawa radhi kufunguka. Tena imeeleza mambo ya ukweli tupu ambayo sisi tulikuwa tunayajua,” kilisema chanzo chetu.IMESEMAJE MITANDAO?Watumiaji mbalimbali wa mitandao ya kijamii wametoa maoni kuwa, kwa asilimia 90 mimba ya Zari si ya Diamond na kuna uwezekano ana tatizo la uzazi kwani hata mpenzi wake wa zamani, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ aliwahi kukaririwa akisema Diamond hajampa ujauzito kama yeye alivyokuwa akijisifia kuwa amempa halafu ukatoka.
Article Source: BongoSwaggz
0 comments:
Post a Comment