DC NJOMBE:MRADI WA KIJANI KIBICHI UWANUFAISHE WAKULIMA WA NJOMBE

Na Gabriel Kilamlya NjombeMkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Amewataka Wakulima na Wataalamu wa Kilimo Wilayani Hapa Kujikita Katika Uzalishaji wa Mboga mboga na Matunda Kutokana na Kuwepo Kwa Fursa ya Soko la Bidhaa Hiyo Baada ya Kusindikwa.Kauli Hiyo Ameitoa Wakati Akizindua Rasmi Mradi wa Kijani Kibichi Mjini Njombe Utakaowasaidia Wakulima Kujikwamua na Kilimo Kupitia Mboga Mboga na Matunda Mradi Ambao Umekuwa Rahisi Kuutekeleza.Bi.Dumba Amesema Kwa Kuwa Lengo la Mradi Huo ni Kutaka Kumnusuru Mkulima Kujikwamu na Hali Duni ya Kipato Basi Hanabudi Kutumia Kilimo Hicho Cha Mboga Mboga na Matunda Kwa Kuendesha Kwa Ubora na Ustadi Mkubwa.Akisoma Taarifa ya Mradi Huo Katibu Mwanzilishi wa Kijani Kibichi Tanzania Michael Uhahula Amesema Kuwa Kupitia Umoja wa Mradi Huo wa Kijani Kibichi Wanaamini Watanzania Wataweza Kunufaika na Kujikwamua na Wimbi la Umasikini.Amesema Hadi Sasa Kumekuwepo na Faida Mbalimbali Ikiwemo Wakulima Kuunganishwa na KujengaMtandao Wao Nje naNdani ya Mkoa,Kukuza Pato la Mtu Mmoja Mmoja Huku Suala la Uhaba wa Fedha na Mitazamo Hasi Miongoni Mwa Jamii Zimetajwa Kuwa ni Changamoto Katika Utekelezaji wa Mradi Huo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: