CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa taarifa yake juu ya utaratibu utakaotumika katika uteuzi wa wagombea ndani ya chama hicho kwa mwaka wa 2015.Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalim ametaja mchakato wa uteuzi kuwa utahusisha hatua tatu katika ngazi ya kata na jimbo auwilaya na hatua moja katika ngazi ya kitaifa.Mwalimu alisema kuwa ngazi yakwanza ni Mkutano Mkuu wa Jimbo ambao utafanyika siku moja kwenye eneo moja au Makao Makuu ya Jimbo au eneoambalo litaamuliwa na vikao vya chama, wagombea kujipigia kura wenyewe na kamati ya utendaji ya jimbo ambayo kazi yake itakuwa ni ya uteuzi wa awali kwa mujibu wa katiba ya chama na kuwasilisha mapendekezo yake kwa Kamati Kuu.Aidha, aliongeza kuwa katika utaratibu huu wa mchakato wa kuwapata wagombea, chama hakitaingilia mamlaka waliyojiwekea na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kwa sasa tayari wale wote wanaohitaji kuchukua fomu za kuwa wagombea, wanaweza kuchukua katika tarehe iliyopangwa.Aliongeza kuwa, fomu hizo zitaanza kuchukuliwa katika majimbo ambayo hayana wawakilishi wao Bungeni ambapo majimbo yenye wawakilishi, fomu zitaanza kutolewa hadi hapo Bunge litakapokuwa limevunjwa na mchakato mzima wa utoaji fomu ukiwa tayari umehalalishwa.Alitaja viwango vya fomu vitakavyotumika katika kugombea ngazi ya urais hadi udiwani kwa upande wa urais ni Sh.1,000,000, ubunge Sh.250,000 pamoja na viti maalum. Udiwani wa kata ni Sh. 50,000 pamoja na udiwani wa viti maalum.Hivyo fomu hiyo itarejeshwa kwenye jimbo au kata ambayo mgombea anagombea na ndipo atapaswa kulipia gharama za fomu husika baada ya kuijaza na pia fomu zitapatikana katika ‘website’ ya chama ambayo niwww.chadema.or.tz
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment