UKATILI:ONA HUYU MWANAFUNZI ALIVYOUAWA BAADA YA KUKUTWA NA BARUA YA MAPENZI

MWANAFUNZI wa Kidato cha Pili, Jofrey Robert Mwakatenya (15) Ameuawa kikatili na baba yake mzazi, Robert Mwakatenya (35) baada ya kumkuta akiwa na barua ya mapenzi, inayodaiwa aliandikiwa na rafiki wake wa kike.Mzazi huyo ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa eneo la Majengo ‘D’ Manispaa ya Sumbawanga, anadaiwa kumwadhibu mwanafunzi huyo, ambaye ni mtoto wake wa kwanza kwa kupiga ngumi na mateke mfululizo kwa zaidi ya saa tatu.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda alithibitisha tukio hilo, lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita. Alisema bado wanamtafuta mtuhumiwa huyo kwani baada ya kufanya kitendo hicho alitokomea.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa Serikali Majengo D, Antony Nyambo alidai kuwa mzazi huyo alikuwa na tabia ya kumwadhibu mwanawe huyo, akimtuhumu kuwa ni mtoro washule .“Nilitaarifiwa juu ya kisa hiki Jumapili saa mbili asubuhi baada ya kutoka katika ibada na raia mwema, ndipo niliamua kufika nyumbani kwa marehemu, nilimkuta akiwa amelazwa chumbani, nilipomfunua niliona akiwa ametapakaa vumbi mwili mzima huku akiwa amevaa nguo ya ndani tu,” alidai mwenyekiti huyo wa mtaa.Inadaiwa kuwa usiku huo wa tukio, mtuhumiwa alianza kumwadhibu kumpiga ngumi na mateke kuanzia saa mbili usiku hadi usiku wa manane.Mtoto huyo baada ya kupata kipigo hicho, alizimia ambapo baba yake alimwagia maji mwilini hadi akazinduka, kisha akamwamuru alale chumbani humo pamoja na mdogo wake.Mzazi wa mtoto huyo alidamka alfajiri na kwenda kwenye chumba walicholala watoto hao na kugundua kuwaJofrey alikuwa mfu.“Ndipo baba huyo alipoaga nyumbani hapo, akidai kuwa anaenda kutafuta gari ili Jofreyaweze kupelekwa hospitalini kwa matibabu. Mzazi huyo hakurudi tena nyumbani kwake hadi sasa,” alibainisha.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: