Lema " ZITTO HANA UBAVU WA KUIGAWA CHADEMA KAMA ANAVYOAMINI,ANAHANGAIKABURE......"

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewatoa hofu wanachama wake mkoani Shinyanga kikidaipropaganda zinazoenezwa na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Bw. Zitto Kabwe, anayedai chama hicho kimepoteza mwelekeo si za kweli bali ni uongo.Mbunge wa Arusha Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa, Bw. Godbless Lema, aliyasema hayo hivi karibuni mkoani Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mahakama ya Mwanzo.Alisema chama chao bado kipoimara na hakitagawanyika kama inavyodaiwa na Bw. Kabwe ambaye CHADEMA kilimfukuza katika chama baada ya kukisaliti hivyo kukiuka Katiba ya chama hicho."Ndugu zangu wana Shinyanga,CHADEMA tupo imara na tutaendelea kuwa imara hadi tukamate dola na kuwakomboaWatanzania ambao wanateseka tangu tupate uhuru."Zitto hana ubavu wa kukigawa chama chetu kama anavyofikirina kuamini...anahangaika bure, alitaka kukiua tukamshtukia na mimi ndiye mtu wa kwanza kubaini njama zake na wenzakeakiwemo Samson Mwigamba na Profesa Kitila Mkumbo; hivyo hawatubabaishi kwa lolote,"alisema.Bw. Lema aliongeza kuwa, Bw. Kabwe alikuwa chanzo cha kufifisha ushindi wa CHADEMAkatika baadhi ya majimbo katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 baada ya kutoa taarifa za uongo kwa wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo ya Katavi, Musoma Vijijini na Singida Mjini na kusababisha wagombea wa CCM wapite bilakupingwa.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chamahicho Taifa (BAVICHA), Patrobass Katambi, aliwataka wanachama wa CHADEMA kusimama imara ili kukiimarisha chama chao na waachane na Bw. Kabwe aliyeonesha dhahiri usaliti wake baada ya kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo."Huyu Bw. Kabwe alikana katakata kujihusisha na Chamacha ACT-Tanzania kama kilivyofahamika awali; lakini siku chache baada ya kutimuliwa CHADEMA akajiunga nacho."Anawadanganya Watanzania kuwa yeye ni mjamaa na moja ya sababu iliyomtoa CHADEMAni kutokuwepo demokrasia ya kweli...kama kweli anathamini demokrasia mbona baada ya kujiunga na ACT ghafla amejitangazia madaraka ya Kiongozi Mkuu wa chama,"alihoji Katambi.Katika hatua nyingine, CHADEMA kimetoa wito kwa wakazi wa Mkoa huo kujitokezakwa wingi ili kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura waweze kupata haki yao ya kuchagua viongozi waadilifu katika Uchaguzi Mkuu.About Glory of Christ Tanzania Church Glory of Christ Tanzania Church (GCTC) is a fast growing church in East and Central Africa with over 70,000 members per one sitting at its main cathedral in Dar es salaam, Tanzania popular knownas “Nyumba ya Ufufuo na Uzima” a Swahili sentence that is is translated in English as “The house of Resurrection and Life”. It was established in 1994 by Pastor Josephat Gwajima who is the founder, Senior pastor and Bishop of the church. GCTC has many branch churches in Tanzania and outside the country Glory of Christ Tanzania Church (GCTC) Ministries GCTC being a Mega Church consists of a number of individual ministries which were carefully made by Pastor Gwajima, the seniorpastor and bishop of GCTC.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: