SHEREHE ZA MEI MOSI 2015 KUFANYIKA KISHAPU MKOA WA SHINYANGA

Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani(Mei Mosi) katika mkoa wa Shinyanga yatafanyika Kesho katika uwanja wa  Uhuru uliopo katika mgodi wa Mwadui wilayani Kishapu.

Mwenyekiti wa Vyama  Huru vya Wafanyakazi –TUCTA mkoa wa Shinyanga Fue Mrindoko(Pichani) amesema sherehe hizo zitaanza saa moja asubuhi kwa maandamano  kutoka jengo la Maendeleo vilivyopo katika mgodi wa Mwadui kuelekea kwenye uwanja wa Uhuru uliopo katika mgodi huo.

Mrindoko amesema mgeni rasmi katika sherehe hizo za Mei Mosi zitakazofanyika kesho Ijumaa anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga.

Amewataka wananchi kujitokeza mapema na kwa wingi katika sherehe hizo ambazo zitahudhuriwa na makundi mbali ya wafanya kazi wa serikali,mashirika ya Umma na Taasisi binafsi.

Mrindoko amesema katika sherehe hizo pia kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo mashindano ya mbio za baiskeli,ngoma,bendi na kuvuta kamba.

Amesema kauli mbiu ya Maadhimisho hayo nchini Tanzania mwaka huu ni “Mfanyakazi Jiandikishe Kura Yako Ina Thamani Kwa Maendeleo Yako”.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: