Maajabu! Msichana
aliyefahamika kwa jina la Dora mkazi wa Magomeni Bagamoyo mkoani Pwani,
hivi karibuni amejikuta akijifungua nazi badala ya mtoto, jambo
lililomshangaza kila mtu.
Ushirikina watajwa
Ilidaiwa kuwa, chanzo
cha Dora kujifungua nazi ni maneno aliyoambiwa na mke mwenzake
aliyefahamika kwa jina la Jamila ambapo aliambiwa hatajifungua kiumbe
cha kawaida na ndipo alipokimbilia Dodoma kukwepa matatizo.
Akizungumza na Amani hivi karibuni akiwa nyumbani kwake Bagamoyo, Dora alisema:
“Nilihamia Bagamoyo nikitokea Mwanza, nikakutana na mwanaume anayeitwa Pascal, tukakubaliana tuishi kama mke na mume.
“Baada ya kukubaliana
hilo, nikapata ujauzito lakini nikashangaa siku moja akaja mwanamke na
kusema yeye ni mzazi mwenzake na Pascal.“Alifanya vurugu, akanijeruhi
kisha akachukua TV na vitu vingine, akaondoka huku akiniambia lazima
nijifungue kiumbe cha ajabu. Nilipata hofu kubwa, mara nikaanza
kusumbuliwa na tumbo, nikapelekwa kwa mganga ambapo niliambiwa
nimerogwa.
Mume wa Dora akihojiwa na mwandishi wa habari (hayupo pichani)
“Nikatibiwa kisha
nikafungwa kitambaa chenye dawa mkononi na kuambiwa nisikivue. “Siku
moja kikapotea kimaajabu, baadaye tukakiona juu ya mti nje ya nyumba.
Nikaachana na masuala ya kienyeji, nikaamua kwenda kanisani, hata hivyo
mauzauza hayakuisha,” alisema Dora na kuongeza:
“Siku uchungu uliponijia
nikiwa Dodoma, ndugu zangu na wakunga wakaja kunisaidia lakini cha
ajabu wakashangaa kuona nazi ndiyo inatoka.“Wakakimbia na kuniacha
nikipandisha mashetani, akaitwa mganga wa kienyeji lakini naye aliogopa
ndipo nikapelekwa kwa walokole kuombewa.
“Nilipopata nafuu na
kurudishwa nyumbani, polisi wakaja na kutuambia eti tumetupa mtoto,
wakasachi hawakuona kitu, wakatupeleka kituoni.“Huko nako nikapandisha
mashetani, nilipotulia nikapelekwa hospitali ambako nilisafishwa lakini
ishu ikawa kubwa, polisi wakatuchukua mimi na mume wangu na kutuweka
ndani, tulitoka baada ya kutoa pesa.
Mfano wa nazi aliyojifungua Dora.
“Cha ajabu niliporudi
nyumbani ili nichukue kadi niende kliniki, nikakuta shanga kibao, ndipo
tukaona cha msingi ni kurudi Bagamoyo na kuhama pale tulipokuwa
tunaishi,” alisema Dora huku akiungwa mkono na mumewe, Pascal.
Imeandaliwa na Chande Abdallah na Deogratius Mongela
0 comments:
Post a Comment