Manyika Jr aomba radhi Simba baada ya kuchafua hali ya hewa

Kipa anayechipukia kwa kasi wa klabu ya Simba, Manyika Peter ‘Manyika Jr’ ameomba radhi kwa ungozi wa klabu, wanachama na mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi mara baada ya kuposti ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa instagram uliowaudhi wanazi wengi wa klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam. Manyika aliposti ujumbe huo baada ya kushutumiwa na mashabiki wa Simba kwamba alicheza chini ya kiwango hali iliyopelekea timu yake kufungwa goli 2-0 dhidi ya Mbeya City mwishoni mwa wiki iliyopita. Kipa huyo ambaye ni mtoto wa golikipa wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania Peter Manyika, aliandika maneno yafuatayo kwenye akaunti yake ya instagram, “anaesema ananiua kiwango aje adake yeye sababu mimi sio kama…..nina haki ya kua na mpenzi kama watu wengine mkihisi sifanyi kazi yenu mniache”, alimaliza huku akiwa ameweka picha ya msichana anaedaiwa kuwa ni rafikiyake wa kike.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: