Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.Sakata la Ufisadi nchini Kenya limechukua sura mpya kufuatia rais Uhuru Kenyatta, kuwasimamisha kazi wakuu wawili wa shirika linalopambana na ufisadi nchini humo, siku mojatu baada ya Bunge kupitisha mswaada inayowalaumu kwa uzembe na utepetevu wa fedha za umma.Kwa mjibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa Ikulu ya Rais Manoah Esipisu,tume ya maadili na kupambana na ufisadi, itaendelea na kazi yake licha ya kusimamishwa kwa wakuu hao wawili.Vigogo hao ni mwenyekiti, Mumo Matemu na naibu wake Bi Irene Keino wamesimamishwa huku uchunguzi ukianzishwa dhidi yao kuhusiana na tuhuma za kuzembea kazini na kutumia vibaya madaraka yao.Hatua hiyo inafuatia chini ya mwezi mmoja baada ya ripoti kutoka kwa tume hiyo kuwasilishwa kwa Rais Kenyatta iliyosababishwa kusimamishwa kazi kwa mawaziri wanne wa serikali ya Uhuru Kenyatta na maafisa wengine 12 wakuu serikalini, huku uchunguzi dhidi yao ukianzishwa
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment