CHAMA CHA ACT TANZANIA CHAIBUKA NA SUALA LA AJALI ZA BARABARANI KUZIDI KUUA WANANCHI

Ili kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na wananchi kupata ulemavu,chama cha ACT wazalendo kimeitaka serekali kutoa taarifa ya tume ya uchunguzi wa ajali za barabarani zilizo fanyiwa utafiti ili kuweza kutafuta namna yakutatua matatizo ya ajali za mara kwa mara. akiwahutubia mamia ya wakazi wa manispaa ya Singida na viunga vyake kwenye mkutano wa kunadi chama cha ACT kiongozi mkuu wa chama hicho Bwana. Zitto Kabwe ,amesema aliyekuwa waziri wa uchukuzi Dk Harsson Mwakyembe aliunda tume ya uchunguzi wa ajali na mpaka sasa majibu hayaja tolewa,jambo ambalo limekuwa likisababisha ajali kuendelea kutokea na kwa kipindi cha mwenzi Mach na April mwaka huu zaidi wa watu mianane wamesha poteza maisha kwa ajili ya ajali. Katika hatua nyingine Bwana. Zitto Kabwe ameitaka serekali kuhakikisha inawabana wamiliki wa mabasi kote nchini ,watoe mikataba ya kazi kwa madereva wao ili waweze kujulikana, kwa kufanya hivyo kuta punguza ajali ambazo siyo za msingi. Awali mwenye kiti wa chama cha ACT Bi.Anna Mghwira na kada wa chama hicho Bwana Selemani Msindi maarufu kwa jina la Afande Sele wamesema huduma nyingi hasa za afya wakati wa zamani zilikuwa zikipatikana kulingana na uwezo wa serikali wakati ule, na kwasasa nchi imekuwa na utajiri mwingi wa madini ,kilimo na biashara,lakini cha kushangaza fursa hizo zimekuwa zikitumiwa na baadhi ya watu na kuwaacha wananchi wengi wakiwa masikini.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: