YANGA YAWEKA WAZI MSIMAMO WAKE KUHUSU BAHANUZI

Uongozi wa Yanga umetamka kuwa, hauna mpango wa kuachana na mchezaji wao, Said Bahanuzi, anayeichezea Polisi Moro kwa mkopo kutokana na uwezo alionao na kiwango kikubwa anachokionyesha kwa sasa. Bahanuzi ambaye alikuwa na maisha ya benchi Yanga, kwa sasa anang’ara na Polisi Moro baada ya kuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo katika safu ya ushambuliaji na kufanikiwa kuifungia mabao matatu mpaka sasa. Hata hivyo, Bahanuzi amebakiza miezi michache kumaliza mkataba wake Yanga na tayari kuna taarifa kuwa baadhi ya timu zimeanza kunyemelea saini yake, hivyo Yanga wameibuka na kuweka wazi misimamo yao hiyo na mchezaji wao huyo kupitia kwa katibu wake, Jonas Tiboroha ambapo alifafanua kuwa hawapo tayari kumuachia kirahisi mshambuliaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar. “Bahanuzi ni mmoja wa wachezaji waliopo kwenye mipango ya benchi la ufundi mpaka sasa na tumemtoa kwa mkopo kwa ajili ya kwenda kuongeza baadhi ya vitu ili msimu ujao akirudi tuweze kumtumia kikamilifu, kwa hiyo bado tunamhitaji, hatupo tayari kumuachia mchezaji kama huyo kama timu nyingine zinavyodhani,” alisema Dk Tiboroha. Pamoja na hayo, taarifa zaidi zinaeleza kuwa, moja ya timu zilizopo kwenye mipango ya kumnyakua straika huyo ni mahasimu wa Yanga, Simba SC.@salehe jembe
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: