AJIBU AMFUATA DIDIER KAVUMBAGU

Straika wa Simba, Ibrahim Ajibu, anayefanya vizuri kwa sasa, ametangaza dhamira yake ya kutaka kutwaa kiatu cha ufungaji bora wa ligi msimu huu, hivyo akatoa tahadhari ya ushindani huo kwa kinara wa mabao mpaka sasa, Mrundi, Didier Kavumbagu anayekipiga Azam FC. Ajibu alifunga ‘hat-trick’ kwenye ushindi wa mwisho wa Simba dhidi ya Prisons wa mabao 5-0 kabla ya mchezo wao wa jana dhidi ya Yanga, akafanikiwa kufikisha idadi ya mabao matano akiwa nyuma kwa mabao manne kwa Kavumbagu mwenye tisa. “Ni kazi kubwa kwenye ligi kama hii kuibuka mfungaji bora lakini kama mtu una nia inabidi kujitahidi zaidi, naamini nitaweza kuchuana na Kavumbagu na wengine wenye mabao mengi mpaka nitimize nia yangu ya kutaka kuwa mfungaji bora msimu huu na kuisaidia timu yangu kukaa kwenye nafasi nzuri,” alisema Ajibu. Wachezaji wengine waliomzidi idadi ya mabao Ajibu ni pamoja na Rashid Mandawa (Kagera-8), Simon Msuva (Yanga-7), Abasirim Chidiebere (Stand-7), wengine ni Samuel Kamuntu (JKT), Ame Ali (Mtibwa), Kipre Tchetche (Azam), wote wana mabao sita
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: