YANGA WAMWAGA MBOGA, WAIGOMEA BODI YA LIGI KUAHIRISHA MECHI KESHO


Uongozi wa Yanga, umeendelea kisisitiza utapeleka kikosi chake uwanjani kesho kwa ajili ya mechi dhidi ya Ruvu JKT.

Yanga imelalama kwamba Bodi ya Ligi imeahirisha mechi hiyo bila kukaa ikazungumza nao halafu ikaipeleka mbele hadi Machi 11 ikiwa ni siku tatu tu kabla ya kuivaa FC Platinum ya Zimbabwe.

Akizumgumza na SALEHJEMBE, Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema watapeleka timu uwanjani na kama mechi haitakuwepo, nao hawatapeleka timu Machi 11.
“Bodi ya ligi inapaswa kuwa wazi kuhusiana na mabadiliko, sisi tuko tayari kucheza kesho. Lakini si Machi 11.

“Angalia siku tatu mbele tuna mechi ya kimataifa, TFF inataka tucheze mechi ya ligi. Kwa nini tusicheze kesho halafu baada ya siku tatu tucheze na Simba.

“Baada ya hapo, tutapata nafasi ya maandalizi ya wiki moja kujiandaa na mechi ya kimataifa ambayo ni muhimu zaidi,” alisema Muro
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: