TIMBE SASA AWAONYA YANGA KUHUSU WAZIMBABWE

Pamoja na kwamba Yanga wameelekeza nguvu zao nyingi kuhusiana na mechi dhidi ya watani wao Simba, Kocha wa Sofapaka, Sam Timbe amewaonya
.


Timbe amewaonya kuhusiana na hatari ya ubora wa kikosi cha FC Platinum ya Zimbabwe ambayo watacheza nayo katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Yanga inakutana na FC Platinum baada ya kuwa imeing’oa BDF XI ya Botswana kwa jumla ya mabao 3-2.

“Yanga wanatakiwa kuwa makini sana, wasidhani wanakutana na timu lelemama. Hata kiwango chao kipo juu.

“Wana kasi, wana wachezaji wanaojitambua na warefu. Pia washambuliaji wao wana uwezo,” alisema Timbe.
“Kingine wanachoweza kupambana nacho ni mipira ya juu, hivyo wawe makini sana.”


Tayari Yanga ipo kambini mjini Bagamoyo kujiandaa na mechi dhidi ya Simba, baada ya hapo maandalizi yatakuwa ni dhidi ya FC Platinum na Ligi Kuu Bara.
@salehe jembe
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: