FILIKUNJOMBE ASHEREKEA NA WANAKIJIJI CHA MADOPE WILAYA YA LUDEWA

Na Njenje habari blog
Ludewa
wazee wa kijiji cha madope wakimchangia fedha mbunge wa jimbo la Ludewa Filikunjombe


Zikiwa ni siku chache zimepita toka wafuasi wa Chadema na Ccm kata ya Kilondo kumchangia kiasi cha Tsh 100,000 kwa ajili ya kuchukua fomu ya ubunge ,Wananchi wa kata ya Madope wilaya ya Ludewa mkoani Njombe nao wamemchangia kiasi cha Tsh 199700 mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa ajili ya kuchukua fomu ya ubunge muda ukifika. Wananchi hao mbali ya itikadi zao za vyama walisema wameunganisha nguvu zao wakiwemo wa vyama vya CCM na Chadema kuchangishana kiasi hicho cha pesa Kama njia ya kutambua mchango wake wa kimaendeleo kwa wana Ludewa. Kada wa Chadema Ernesto Mgaya alisema yapo maeneo ambayo bado watu wanavutana kisiasa na ni vigumu kwa wana Ccm na Chadema kukutana katika mkutano mmoja wa siasa ila si Ludewa ambako itikadi za vyama. Kwani alisema wananchi walipochagua mbunge walitaka maendeleo si vinginevyo na kutokana na maendeleo Makubwa yaliyopo Ludewa kwa sasa hawahitaji tena siasa za vyama zaidi ya siasa za kimaendeleo . Wananchi hao waliyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kijijini hapo ulioambatana na zoezi la mbunge huyo kuunga mkono jitihada za wananchi hao katika Ujenzi wa zahanati ya kijiji kwa kukabidhi vifaa vya Ujenzi zikiwemo bati ,saruji,rangi na Magodoro vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh Milioni 5.2 " Awali ludewa kulikuwa na mvutano mkubwa wa kisiasa Kati ya Chadema na CCM ila toka amekuwa mbunge Filikunjombe ....wananchi wote tumeungana na kuweka vyama vyetu kando na kuunga mkono jitihada za mbunge wetu katika kuleta maendeleo ya Ludewa "alisema kada huyo wa Chadema Kwa upande wao wazee wa kijiji hicho walisema Ludewa imekuwa na wabunge wengi zaidi ya watano ila Kati Yao hakuna aliyeweza kuleta maendeleo kwa muda mufupi Ludewa Kama Filikunjombe na kusema sadaka Yao kwa ajili ya kufanikisha nauli na gharama ya fomu ni Moja Kati ya kielelezo tosha kwa wana Ccm wanaotaka ubunge kuwa Ludewa hawahitaji mtu zaidi ya mbunge wao Filikunjombe. Wazee wa kijiji hicho cha Madope walisema katika mchakato wa kura za maoni mwaka 2010 wengi wao hawakuwa upande wa Filikunjombe kutokana na kutokuwa na imani kutokana na umri wake ila kwa sasa wamebaini umri si kigezo cha kushindwa kuleta maendeleo Hivyo walisema kwa uchaguzi huu hakuna wasiwasi wowote juu ya mbunge huyo bali ajipange kwa kusherekea ushindi wa kimbunga dhidi yake. Kwa upande wake Filikunjombe alisema kero kubwa ya kijiji hicho ni kituo cha afya hali iliyopelekea wananchi wengi kuchukia chama tawala kutokana na kukosekana kwa huduma ya afya Kijijini hapo ila kero hiyo kaifanyia Kazi kwa kutoa vifaa vyote vya ujenzi na fundi wa kusimamia ujenzi huo . Hata hivyo Filikunjombe alisema zipo baadhi ya changamoto ambazo wananchi wamekuwa wakizihitaji kutatuliwa ambazo kwa sasa zinahitaji muda na kuzifanyia utekelezaji zile za msingi zaidi Kama kituo cha afya na maji Kabla ya kujenga kituo cha polisi. " Katika Risala yenu mmeorodhesha changamoto mbali mbali ikiwemo ya kituo cha afya,maji,na kituo cha Polisi na Mimi si mbunge wa kudanganya naomba kwa sasa tuanze kituo cha afya kwanza na baadae maji pia kituo cha polisi ....lazima tuanze jambo moja Moja tukuenda na yote kwa wakati mmoja tutakwama" alisema Filikunjombe mwisho
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: