RC-NJOMBE ATANGAZA KUPAMBANA NA WAFANYABIASHARA WANAOENDELEA KUFUNGA MADUKA

Kitendo Cha Wafanyabiashara Kufunga Maduka Yao Kwa Kile Wanachodai ni Kuwaunga Mkono Wafanyabiashara Wenzao Akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Taifa Johnson Minja Pindi Anapokwenda Mahakamani Kimeikasirisha Serikali Mkoani Njombe. Aidha Hatua Hiyo Imemfanya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi Kutoa Tamko la Kuwataka Wafanyabiashara Hao Kufungua Haraka Maduka Yao na Kuendelea na Biashara Kutokana na Athari Kubwa Zinazowakumba Wananchi. Dokta Nchimbi Ametoa Kauli Hiyo Kufuatia Wafanyabiashara Mkoani Njombe Kufunga Maduka Yao Hapo Machi Tatu Mwaka Huu Wakidai Wanakwenda Mahakamani Kusikiliza Kesi ya Mfanyabiashara Mwenzao Mexon Sanga na Leo Wakidai Kumuunga Mkono Mweyekiti wa JWT Johnson Minja Jambo Ambalo ni Kero Kubwa Kwa Wananchi. Amesema Kitendo Hicho Kinasikitisha na Kinawanyima Haki Wananchi Pindi Wanapofika Dukani na Kukuta Maduka Yamefungwa Ilihali Wamekubali na Serikali Kufanyabiashara Hizo. Kutokana na Adha Hiyo Amewataka Wafanyabiashara Hao Kufungua Maduka Yao Haraka Iwezekanavyo Huku Akiahidi Kuwachukulia Hatua Kali Wale Wote Watakaoonekana Kuwa Chanzo Cha Wafanyabiashara Hao Kuendelea Kufunga Maduka Yao. Hata Hivyo Amekitaka Chama Cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo TCCIA Kulifikiria Kwa Kina Suala Hilo Ili Kufikia Hatima ya Kufungua Maduka Hayo Haraka Iwezekanavyo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: